• Nairobi
  • Last Updated October 1st, 2023 9:40 PM
Mwanamume auawa na umati akidaiwa kuiba mihogo   

Mwanamume auawa na umati akidaiwa kuiba mihogo  

Na ALEX KALAMA

MWANAMUME alifariki Jumatatu katika kijiji cha Patanani kilichoko Shimba Hills, Kaunti ya Kwale baada ya kupigwa na umati akidaiwa kuiba mihogo shambani.

Kulingana na ripoti ya polisi, wananchi walimkamata Mwero Muzi, 45, na kumuua papo hapo.

Mkuu wa polisi eneo la Tiribe Kassim Ko amesema kuwa alifahamishwa kuhusu tukio hilo na wananchi.

Ameonya wananchi hao akiwataka wasiwe wakijichukulia sheria mikononi.

“Ni kweli nilipata habari kuwa kuna mwanamume ambaye ameuawa na raia baada ya kufumaniwa akiiba mihogo, na ninaonya umma ufuate mkondo wa sheria ila si kuchukua sheria mikononi mwao,” alitahadharisha Bw Khoi.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Kaunti Ndogo ya Kinango.

 

  • Tags

You can share this post!

Dai mganga alishauri washukiwa wafunike Sh700, 000 za wizi...

Bangi imeharibu ‘transfoma’ za vijana wengi...

T L