• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 8:50 AM
Tumewafaa wateja wetu wakati wa corona  – Safaricom

Tumewafaa wateja wetu wakati wa corona – Safaricom

Na WANGU KANURI

[email protected]

Kupitia ripoti endelevu ya kibiashara iliyochapishwa na Safaricom juzi, kampuni ilisema imewapiga jeki wateja wao.

Hii ni kwa kuanzisha ofa mbalimbali ili kurahisisha mawasiliano na maendeleo ya kazi na mabiashara. Huduma za tunukiwa kwa mfano ziliwapa watu fursa ya kuendelea kushirikiana na wenzao. Hii ilikuwa kwa kuchagua ofa ya tunukiwa data au tunukiwa ujumbe mfupi au tunukiwa saa za kubonga.

Isitoshe, Safaricom iliwapa wateja hao nyongeza ya 500MBs bure ambayo ilikuwa ikiisha saa sita usiku. Hali kadhalika, ili wateja waweze kuwasiliana hata kama hawana data, Safaricom ilianzisha huduma ya Facebook Kadogo.

Sababu serikali iliamuru shule zote kufungwa, Safaricom ilihakikisha wanafunzi wamepata elimu hata wakiwa manyumbani. Hii ilikuwa kupitia ushirikiano wa Safaricom na Longhorn, Viusasa Elimu, Shupavu-Eneza na Taasisi ya Ukuzaji Mitaala nchini (KICD).

“Vile vile, wanafunzi ambao walitaka kupata maarifa kuhusu masomo ya Sayansi, Teknolojia, Injinia na Hisabati (STEM), waliwezeshwa kukikata kiu chao cha masomo kupitia ujumbe mfupi. Hii iliwezeshwa na ushirikiano wa Safaricom na UNESCO pamoja na Eneza Shupavu 291 Solution,” ripoti hiyo ikaonyesha.

Hali kadhalika, malipo ya kutoa au kutuma pesa chini ya Sh1,000 iliondolewa mpaka Disemba 31st mwaka jana huku wateja 105,604 waliokuwa na tili amilifu ya M-pesa wakipata Sh200 milioni za kuwasaidia kununua viyeyushi.

“Safaricom ilianzisha Bonga for Good. Mradi huu uliwawezesha wateja kutumia pointi zao za Bonga na kulipia bidhaa au hata kuzipatiana kwa wenzao. Hivi sasa huduma hii ni ya kudumu na wateja wanaweza kuzilipia bidhaa zao kwa kutumia pointi za bonga katika kila tili ya Buy Goods nchini,” Safaricom ikaandika.

You can share this post!

SHAIRI: Msichana ni muhimu, heri kumsaidia

Tumejifunza kutokana na makosa yetu ya zamani , KANU Fresh...