• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 11:30 AM
Wanafunzi wa vyuo wanavyomezea mate mijibaba

Wanafunzi wa vyuo wanavyomezea mate mijibaba

NA RICHARD MAOSI

WAMILIKI wa vilabu wanalalamikia ongezeko la idadi ya mabinti wa vyuo vikuu Nairobi wanaotembea na wanaume wazee rika ya baba zao, wakiishia kushiriki mapenzi.

Wanapenda kujivinjari na wazee au watu maarufu, wakiamini kuwa watawasaidia kupata kazi baada ya kuhitimisha shule.

Meneja wa Klabu moja eneo la Westlands aliambia Taifa Leo Dijitali kwamba mabinti wa vyuo wanavutiwa na uwezo mzuri wa kiuchumi, na vilevile wanaweza kuwatimizia mahitaji yao yote ya kimsingi kama vile kuwalipia kodi ya nyumba.

“Ukizuru vilabu vingi katika maeneo ya Westalands, nyakati za usiku utafikiri ni baba na binti yake,” akasema mjuzi wetu.

Anasema wao hutumia mitandao ya kijamii kuunganishwa na wanaume hao kwa ada inayochezea kati ya Sh500 hadi 1, 000.

“Kuna mawakala maalum ambao ndio hufanya kazi ya kutuunganisha na wanaume hao. Mabinti hawajutii kwa sababu wazazi huwapatia hela kidogo sana za matumizi.”

Aidha, wahudumu wa mikahawa pia wanatumika kwa asilimia kubwa kuwaunganisha akina dada hao na wanamume.

Warembo wengi wana zaidi ya mchumba mmoja na wanaishi maisha ya kifahari, ambayo ni ya kupigiwa upatu.

Taifa Leo Dijitali imetambua baadhi ya wanaume kutoka Nairobi wanajificha katika mitaa ya kifahari ya Malindi au Naivasha, hasa msimu huu wa sherehe za mwisho wa mwaka wakati ambapo mabinti wengi wanaelekea nyumbani, baada ya kufunga vyuo.

Baadhi walifunga shule kitambo na inasemekana hawajarejea nyumbani kwa minajili ya kujivinjari kwanza.

  • Tags

You can share this post!

Samidoh ampa mfuasi wake tonge la majibu

Raila: Utawala wa kimikoa ufutiliwe mbali

T L