• Nairobi
  • Last Updated May 24th, 2024 2:08 PM
Wanaonitaka wamesota kama mimi, hawawezi kunisaidia na chochote!

Wanaonitaka wamesota kama mimi, hawawezi kunisaidia na chochote!

SHANGAZI,

Mwanamume anayenitaka hawezi kugharamia mahitaji yangu ya pesa, anatafuta kazi kama mimi tu. Kuna wengine wengi walio tayari kunisaidia lakini wana familia. Nifanyeje?

Naelewa kwamba unataka mpenzi aliye na uwezo wa kugharamia mahitaji yako ya pesa. Lakini achana na waume wa wenyewe. Wapo walio na uwezo na ambao hawajaoa. Endelea kutafuta.

Dume la kwangu linalemewa chumbani!

Mpenzi wangu ni barobaro wa miaka 39. Ajabu ni kuwa analemewa na kazi chumbani. Nimeshauriana naye kuhusu jambo hilo lakini ananilaumu akisema mimi ndiye sitosheki. Nifanyeje?

Si rahisi kwa mwanamume kuungama kuwa ana upungufu wa aina hiyo na ndiyo sababu anakulaumu wewe. Iwapo unaamini hali yake hiyo itakuwa changamoto katika uhusiano wenu ni heri muachane utafute anayekufaa.

Hajawahi kuniambia neno ‘ninakupenda’

Mwanamume mpenzi wangu hajawahi kutamka penzi lake kwangu. Nilimfungulia moyo wangu kwanza na akakubali. Sijui kama kweli ananipenda ama alikubali kunifurahisha. Nina wasiwasi.

Si jambo la kawaida kwa mwanamke kumtongoza mwanamume. Inawezekana mwanamume huyo hakupendi lakini aliona aibu kukwambia. Ni muhimu umuulize ili ujue ukweli.

Mahitaji ya mpenzi wangu sasa yanilemea

Nina mpenzi na nampenda kwa dhati. Nimejinyima mambo mengi ili kumsaidia kifedha. Lakini naona mahitaji yake yanazidi kuongozeka na nimeanza kulemewa. Nifanyeje?

Ni vyema kumfaa mpenzi wako kwa hali na mali. Hata hivyo, huo si wajibu wa lazima bali ni hiari. Ukiwekeza pesa nyingi kwake kisha akuache utaachwa ukijuta. Msaidie kulingana na uwezo wako.

  • Tags

You can share this post!

Raha ya mjane mchanga wa Kibor wakili akiambia korti...

Majina ya watoto 131 walioangamia Shakahola yajulikana kesi...

T L