• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 6:50 PM
Wanaraga wa Chipu waingia kambini Brookhouse dimba la Afrika likinukia

Wanaraga wa Chipu waingia kambini Brookhouse dimba la Afrika likinukia

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya taifa ya raga ya wachezaji 15 kila upande ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 maarufu Chipu, itaingia leo kambini kwa ajili ya Kombe la Afrika litakaloanza Juni 26.

Mabingwa wa zamani Namibia waliratibiwa kuwa timu ya kwanza kuingia kambi hiyo katika Shule ya Brookhouse mnamo Jumapili usiku baada ya kupiga abautani kuhusu kutoshiriki mashindano haya. Zaidi ya wiki moja iliyopita, vyombo vya habari nchini Namibia viliripoti kuwa Namibia imejiondoa mashindanoni.

Chipu ya kocha Curtis Olago imekuwa ikifanyia mazoezi yake mjini Nakuru na uwanjani RFUEA jijini Nairobi kwa zaidi ya majuma matatu. “Senegal itawasili Juni 23 nayo Madagascar hapo Juni 24,” Shirikisho la Raga Kenya (KRU) lilisema jana. Kenya itaanza kampeni yake dhidi ya Senegal (Juni 26), Madagascar (Juni 29) na Namibia (Julai 3).

Kombe hilo maarufu kama Barthes Trophy litafanyika Juni 26 hadi Julai 3 katika uga wa kitaifa wa Nyayo. Lilifaa kuandaliwa Machi 25 hadi Aprili 4, lakini likaahirishwa kutokana na masharti ya kudhibiti wimbi la tatu la covid-19.

  • Tags

You can share this post!

Shujaa na Lionesses kufahamu makundi yao ya Olimpiki

NAPSA Stars wanayochezea Wakenya Calabar na Odhoji yalemewa...