• Nairobi
  • Last Updated June 12th, 2024 4:24 PM
Washtakiwa kwa wizi wa samaki

Washtakiwa kwa wizi wa samaki

Na RICHARD MUNGUTI

VIBARUA watatu wameshtakiwa kwa wizi wa samaki wa thamani ya Sh30, 000.

Jesse Mwangi, Paul Kimathi na Samuel Okello walishtakiwa mbele ya hakimu mwandamizi Bi Agnes Mwangi.

Walikanusha kuiba samaki hao mnamo Mei 17, 2023.

Samaki hao walikuwa wa mfanyabiashara John Waithaka.

Mahakama ilielezwa kwamba watatu waliiba samaki hao walipoachwa katika steji ya Mihango, mtaani Kayole.

Mbali na shtaka la wizi, watatu hao walikabiliwa na kupatikana wakiwa na baadhi ya samaki hao wakijua wameibwa ama kupatikana kwa njia isiyo halali.

Bw Waithaka alikuwa amenunua samaki hao katika soko la wazi la Gikomba na kupeana kwa matatu impelekee Mihango.

Washtakiwa waliachiliwa kwa dhamana ya Sh15, 000 hadi Julai 18, 2023 kesi itakapoanza kusikizwa.

  • Tags

You can share this post!

Amerika yaadhibu spika wa Uganda kwa kupitisha sheria...

Mwanamke mashakani kwa kuficha ‘dume’ mbakaji

T L