• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 6:50 PM
Wolves wamteua kocha Bruno Lage kujaza pengo la mkufunzi Nuno Espirito

Wolves wamteua kocha Bruno Lage kujaza pengo la mkufunzi Nuno Espirito

Na MASHIRIKA

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

WOLVES wamemteua kocha Bruno Lage kujaza pengo la mkufunzi raia wa Ureno, Nuno Espirito Santo ambaye alibanduka rasmi ugani Molineux, Uingereza mwishoni mwa msimu wa 2020-21.

Lage ambaye pia ni raia wa Ureno, aliagana na klabu ya Benfica ya Ligi Kuu ya Ureno mnamo Juni 2020 baada ya kudhibiti mikoba ya kikosi hicho kwa kipindi cha miezi 18.

Lage, 45, alitua nchini Uingereza mnamo Mei 25, 2021 na akaandaa kikao cha faragha na mwenyekiti wa Wolves, Jeff Shi pamoja na mkurugenzi wa benchi ya kiufundi, Scott Sellars. Ni wakati huo ambapo aliafikiana na usimamizi kutwaa mikoba ya Wolves inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Nuno aliagana rasmi na Wolves mnamo Mei 23, 2021 baada ya kuhudumu ugani Molineux kwa kipindi cha miaka minne akijivunia kuchangia pakubwa uthabiti wa kikosi hicho tangu kipandishe ngazi kushiriki soka ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwa mara ya kwanza mnamo 2018.

Lage aliwahi kuwa msaidizi wa kocha Carlos Carvalhal kambini mwa Sheffield Wednesday na Swansea City. Akidhibiti mikoba ya Benfica, aliongoza kikosi hicho kutia kapuni taji la Ligi Kuu ya Ureno mnamo 2019.Kuajiriwa kwake na Wolves kunasukumwa zaidi na wakala maarufu, Jorge Mendes ambaye pia ni ajenti wa Nuno.

Chini ya Nuno, Wolves walikamilisha kampeni za EPL katika nafasi ya saba mnamo 2018-19 na 2019-20. Kikosi hicho kiliambulia nafasi ya 13 mnamo 2020-21 kwa alama 45 sawa na Newcastle United.“Nimefurahi kujiunga na kikosi hiki ambacho kina matamanio makubwa katika soka ya Uingereza na bara Ulaya,” akasema Lage.

  • Tags

You can share this post!

Bondia Okwiri kupigania mamilioni Agosti, Mike Tyson...

Timu ya Kenya ya Olimpiki yapokea chanjo ya pili ya Covid-19