• Nairobi
  • Last Updated April 17th, 2024 5:55 PM
Kinaya kandarasi za EACC zikitiliwa shaka

Kinaya kandarasi za EACC zikitiliwa shaka

Na LEONARD ONYANGO

TUME ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) ni miongoni mwa taasisi za serikali zilizo na madeni ya wanakandarasi hewa.

Kulingana na ripoti iliyotolewa na Tume ya Ugavi wa Mapato (CRA), EACC ilikuwa inadaiwa Sh16.7 milioni zinazotiliwa shaka kufikia Juni 30, 2021.

Hiyo ni kwa sababu hakuna stakabadhi za kuonyesha kwamba EACC ilipata huduma au bidhaa zilizoagizwa.

Ripoti hiyo huenda ni ishara kwamba huenda kuna uozo wa ufujaji wa fedha za umma ndani ya EACC licha ya kutwika jukumu la kukabiliana na wafisadi.

Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa Shirika la Habari la Taifa (KBC) linazongwa na deni kubwa la Sh370 milioni na hakuna stakabadhi za kuthibitisha kandarasi hizo.

Idara ya magereza, Hazina Kuu ya Kitaifa, Idara ya Mipango, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Wizara ya Michezo, Wizara ya Madini na Utalii ndizo serikali zilizo na madeni yanayotiliwa shaka.

Idara ya magereza, kwa mfano, inadaiwa Sh15 milioni lakini hakuna stakabadhi za kuthibitisha kandarasi zilizotolewa.

Hazina Kuu ina deni la Sh4 bilioni linalotiliwa shaka, Idara ya Mipango (Sh3.6 milioni), Michezo (Sh66 milioni), IEBC (170 milioni) na Utalii (Sh1.7 milioni).

Idara za serikali na tume zinadaiwa jumla ya madeni hewa ya Sh653 milioni ambayo yanatiliwa shaka.

Kwa ujumla serikali ya kitaifa inadaiwa jumla ya Sh36.4 bilioni – kiasi ambacho kinajumuisha madeni hewa na madeni halali yaliyo na stakabadhi za kuthibitisha.

Ofisi ya Rais, inayojumuisha afisi ya Naibu Rais, inadaiwa madeni halali ya Sh121 milioni.

Wizara ya Usalama wa Ndani inayoongozwa na Dkt Fred Matiang’i haijalipa wanakandarasi kitita cha Sh 681 milioni.

You can share this post!

KINA CHA FIKIRA: Elimu bila nasaha kwa wanafunzi ni bomu...

CHEPKWONY: Wanafunzi wapewe fursa ya kujieleza, washauriwe

T L