• Nairobi
  • Last Updated November 28th, 2023 7:53 PM
Kibra itakuwa sawa na mtaa wa kifahari wa Karen, Ruto aahidi

Kibra itakuwa sawa na mtaa wa kifahari wa Karen, Ruto aahidi

NA SAMMY WAWERU

RAIS William Ruto ameahidi Jumapili, Oktoba 1, 2023 kwamba analenga kugeuza mtaa wa mabanda wa Kibra, Jijini Nairobi kuwa mtaa wa kifahari.

Kiongozi wa nchi alisema, chini ya kipindi cha miaka 10 ijayo mtaa huo ambao tangu Kenya ijinyakulie uhuru majengo yake yamekuwa ya mabanda, utakuwa sawa na mitaa mingine ya kifahari nchini.

“Chini ya miaka 10 ijayo, Kibra haitajulikana kama mtaa wa mabanda tena. Utakuwa mtaa wa kifahari,” Dkt Ruto akasema.

Alisema hayo alipohudhuria ibada ya misa katika Kanisa la Deliverance International, Lang’ata, Nairobi.

Alikuwa ameandamana na baadhi ya viongozi wa kisiasa waliochaguliwa Kaunti ya Nairobi, ambapo aliahidi kuwa mtaa wa Kibra utakuwa kama Karen, Kileleshwa, Lavington, na mitaa mingineyo ya kifahari nchini.

Alisema lengo hilo ataliafikia kupitia mpango wake wa nyumba za bei nafuu unaoendelezwa.

Wafanyakazi nchini wanapitia makato ya asilimia 3, nusu yake ikigharamiwa na mwajiri kwa minajili ya programu ya nyumba za bei nafuu.

Kinaya hata hivyo, Rais Ruto alisema Jumapili kwamba mpango huo shabaha yake si kuwa na nyumba nyingi ila ni kusaidia vijana kupata nafasi za kazi.

Chini ya serikali ya mseto iliyoongozwa na Rais Mstaafu, Mwai Kibaki ambaye kwa sasa ni marehemu, kwa ushirikiano na kinara wa ODM, Bw Raila Odinga, sehemu ya Kibra kulijengwa majumba ya kisasa.

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, pia alikuwa na mpango wa nyumba za bei nafuu.

 

  • Tags

You can share this post!

Ugumu wa maisha wasukuma wanafunzi wa vyuo kuishi kama mume...

Stephen Letoo apamba siku maalum ya kuzaliwa kwa Chemutai...

T L