• Nairobi
  • Last Updated February 29th, 2024 5:13 PM
Lamu yaongoza kwa ajali za mashua baharini – ripoti

Lamu yaongoza kwa ajali za mashua baharini – ripoti

Na KALUME KAZUNGU

KAUNTI ya Lamu iliongoza kwa idadi kubwa zaidi ya watu waliokufa maji kwenye Bahari Hindi eneo la Pwani katika mwaka 2021.

Kulingana na ripoti ya Halmashauri ya Kudhibiti Vyombo vya Baharini nchini (KMA), jumla ya watu 11 walifariki ilhali wengine 166 wakiokolewa kwenye ajali za boti na mashua zilizotokea baharini eneo la Lamu kati ya Januari na Disemba 2021.

Idadi hiyo ya vifo na majeruhi kutokana na ajali za vyombo vya baharini Lamu ndiyo ya juu zaidi kurekodiwa ikilinganishwa na kaunti nyingine zote za Pwani.

Mbali na Lamu, Pwani iko na kaunti za Mombasa, Kilifi, Kwale, Taita Taveta na Tana River.

Uchunguzi uliofanywa na Taifa Leo ulibaini kuwa mbali na Lamu, baadhi ya kaunti za Pwani zilirekodi vifo visivyozidi kumi na majeruhi wasiozidi ishirini baharini ilhali nyingine zikikosa kurekodi vifo vyovyote.

Mnamo Agosti 2021, kaunti ya Kilifi ilirekodi vifo 7 katika ajali moja pale boti ya mabaharia 15 kutoka visiwa vya Comoros ilipozama baharini eneo la Watamu baada ya kushindwa kustahimili mawimbi makali.

Mabaharia wanane waliokolewa kwenye ajali hiyo.

Mwezi Agosti ndio uliokuwa mbaya zaidi kwa kaunti ya Lamu kwani uliandikisha ajali 12 za mashua, nyingi zikiwa ni za wavuvi ilhali watu 7 wakifariki mwezi huo kutokana na ajali hizo za baharini.

Mkurugenzi Mkuu wa KMA, Robert Njue, alisema katika harakati za kuimarisha usalama wa baharini, halmashauri hiyo imekuwa ikiendeleza mafunzo mbalimbali ya ubaharia kwa manahodha kaunti ya Lamu na maeneo mengine ya Pwani na nchini, ambapo wanaohitimu wamekuwa wakipokezwa vyeti.

  • Tags

You can share this post!

Bei ya unga kupanda wakulima wakikwamilia mahindi

Azimio la Raila lamtikisa Ruto

T L