• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 2:11 PM
Polisi bandia anayehangaisha wakazi Nairobi

Polisi bandia anayehangaisha wakazi Nairobi

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAMUME anayejifanya polisi na kuhangaisha wakazi jijini Nairobi amekamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Polisi bandia huyo aliyetambuliwa kama Stanley Ng’ang’a, alishtakiwa mbele ya hakimu mkazi Mercy Malingu.

Ng’ang’a anakabiliwa na shtaka la kukamata mfanyabiashara Nairobi, akijifanya askari.

Akisomewa makosa yake mbele ya Hakimu Mercy, alikana kuwatia nguvuni Kenton Ombati pamoja na wafanyakazi wake wawili.

Ng’ang’a alidaiwa alidai apewe hongo ya Sh10, 000 ndipo awaachilie.

Lakini kitumbua chake Ng’ang’a kiliingia mchanga polisi kutoka kituo cha Kamkunji walipofika katika afisi ya Ombati iliyoko katika jengo la Simba Centre eneo la River Road, Nairobi.

Ng’anga alijifanya alikuwa afisa wa polisi kutoka kituo cha Central alipomkamata Ombati.

Hakimu alielezwa kwamba katika harakati za kuwakamata Ombati na wafanyakazi wake wawili, mshtakiwa aliwajeruhi.

Wakili wa Ombati aliomba mahakama imwachilie mshtakiwa kwa kiwango cha juu cha dhamana.

Bi Malingu alimwamuru mshtakiwa alipe dhamana ya Sh500,000 kabla ya kuachiliwa kutoka gerezani.

Kesi itasikizwa Septemba 11, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Kisumu All Starlets kukwaana na Ulinzi Starlets kwenye...

Wanafunzi South B PEFA Academy wachagua viongozi...

T L