NA MAUREEN ONGALA
POLISI Kilifi wameomba mahakama kuwapa siku 14 kuwazuilia wanachama 10 wa ‘Kanisa la Mungu, Neno la Kweli’ ambao walikamatwa kwa madai kwamba walihusika kwa vifo vya watoto wawili.
Hakimu Mwandamizi Mkuu wa Kilifi Justus Kituku anatarajiwa kutoa uamuzi mnamo Alhamisi, Septemba 21, 2023.