• Nairobi
  • Last Updated October 2nd, 2023 7:00 AM
Stephen Lenamarle achaguliwa Spika mpya wa Samburu

Stephen Lenamarle achaguliwa Spika mpya wa Samburu

NA GEOFFREY ONDIEKI

MHESHIMIWA Stephen Lenamarle amechaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Kaunti ya Samburu.

Bw Lenamarle amepata kura 23 kati ya 25 kwenye raundi ya kwanza ya upigaji kura, akimbwaga mpinzani wake Dkt Josephine Kulea.

Wakati wa upigaji kura, mirengo mikuu ya Kenya Kwanza na Azimio imeonyesha utulivu bila kushuhudiwa vuta nikuvute.

Bw Lenamarle anachukua nafasi hiyo iliyoachwa wazi baada ya Fred Lengees kujiuzulu mnamo Mei 16, 2023.

Bw Lengees aliwasilisha ombi la kujiuzulu ili kuchukua wadhifa mpya katika Idara ya Usalama ya Umoja wa Mataifa.

  • Tags

You can share this post!

Haji sasa atetewa na wabunge kutoka jamii za wafugaji

Bellingham atawazwa Mchezaji Bora wa Bundesliga 2022-23

T L