• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 11:30 AM
Vijana waonywa dhidi ya ngono bila kinga

Vijana waonywa dhidi ya ngono bila kinga

NA WINNIE ATIENO

NAIBU Gavana wa Taita Taveta Bi Christine Kilalo amesema serikali ya kaunti itashirikiana na washikadau wa afya ili kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi.

Bi Kilalo alisema serikali ya Kaunti ya Taita Taveta itaendeleza uhamasisho kuhusu ugonjwa huo na namna ya kuepuka au kuishi na virusi.

Hata hivyo, alionya vijana dhidi ya kujihusisha na ngono bila kinga akisema inaongeza maambukizi mapya.

“Maambuziki mapya yanayonakiliwa yanatokana na tabia za vijana kujihusisha na ngono kiholela holela,” alisema Bi Kilalo.

Vile vile alisema serikali ya kaunti itaongeza uwezo wa hospitali za umma ili wahudumu wa afya waweze kuendelea kutoa huduma za Ukimwi.

Kaunti hiyo ilitaja sehemu tatu ambapo maambukizi yanaenezwa zaidi ikiwemo katika sekta ya madereva wa masafa marefu, sehemu za uchimbaji migodi na sokoni hasa katika eneo la Taveta.

 

  • Tags

You can share this post!

Serikali yalenga kukusanya Sh4.2 bilioni kila siku

Polo na kahaba wakwamiliana lojing’i Othaya

T L