• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 4:47 PM
Washukiwa saba wanaswa kwenye operesheni dhidi ya pombe haramu, mitambo ya kamari

Washukiwa saba wanaswa kwenye operesheni dhidi ya pombe haramu, mitambo ya kamari

NA SAMMY KIMATU

POLISI katika eneo la Makadara wameendeleza vita dhidi ya pombe haramu ambapo kwenye operesheni ya hivi punde wamenasa washukiwa saba.

Kando na hayo, polisi wamefanikiwa kunasa mashine mbili za kamari.

Naibu kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Makadara, Bw Dennis Omuko ameambia Taifa Leo kwamba msako wa Jumanne umeendeshwa na polisi kutoka kituo cha South B.

“Polisi walifanya msako katika mtaa wa Hazina na kunasa mshukiwa mkuu anyeuzia watu pombe haramu ya chang’aa pamoja na washukiwa waliokuwa ndani ya nyumba yake wakinywa,” Bw Moruko akasema.

Aliongeza kwamba washukiwa hao wamefunguliwa mashtaka na wanatarajiwa kufikishwa kortini Jumatano.

Kadhalika, Bw Omuko aliongeza kwamba operesheni zaidi zinaendelea akieleza kwamba nyumba zinazopatikana na pombe aina ya chang’aa ndizo pia zinatumiwa na wahalifu kama maficho yao.

  • Tags

You can share this post!

Akothee: Msiniulize kuhusu wadhifa wangu wa Rais wa...

PATA USHAURI WA DKT FLO: Nahisi maumivu kila ninapoenda...

T L