• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 2:11 PM
Ada ya kujipatia paspoti yaongezwa huku Ruto akiwinda pato zaidi la kuendesha Serikali

Ada ya kujipatia paspoti yaongezwa huku Ruto akiwinda pato zaidi la kuendesha Serikali

NA MWANDISHI WETU

Mahakama Kuu imepiga breki utekelezwaji wa tangazo la Gazeti Rasmi la Serikali lililochapishwa Novemba 7, 2023 ambalo liliongeza ada katika huduma mbali mbali ikiwemo upataji kitambulisho cha kitaifa na paspoti.

Hatua hiyo imejiri baada ya mkazi wa Nakuru, ambaye ni daktari kufika mahakamani kupinga nyongeza hizo ambazo zilipata Wakenya katika hali ya kutozitarajia.

Kulingana na tangazo hilo lililotiwa saini na Waziri wa Usalama na Mambo ya Ndani Profesa Kithure Kindiki, kujipatia paspoti ya kawaida, ya kurasa 34 itakuwa Sh7,500 kutoka Sh4,500 ambayo Wakenya wamekuwa wakilipa kwa miaka mingi. Ile ya kurasa 66 nayo imetoka Sh7,500 hadi Sh12,500.

Kujipatia kitambulisho cha kawaida ambapo Mkenya hajakuwa akitozwa ada yoyote, tangazo hilo lilisema mtu atakuwa anatozwa Sh1,000. Hii ilimaanisha kwamba Mkenya yeyote anayetimu umri wa miaka 18 atahitaji kutafuta Sh1,000 kujipatia kitambulisho cha kitaifa ambacho kinahitajika katika huduma zote ikiwemo kujipatia laini ya Mpesa na pia kupiga kura.

Huduma zingine kama vile kujipatia kitambulisho baada ya kilichokuwepo kupotea, pia imeongezwa kutoka Sh100 hadi Sh2,000 huku kuandikisha mtoto aliyezaliwa ili apate cheti cha kuzaliwa, pamoja na kujipatia cheti cha kuaga dunia kwa mpendwa pia kukiongezwa ada.

Haya yanajiri wakati ambapo serikali ya Rais William Ruto imeleta mabadiliko makubwa haswa katika ulipaji ushuru na uongezeaji ada katika huduma nyingi nchini.

Yanajiri pia wakati ambapo mamilioni ya Wakenya wanalalamikia hali mbovu ya uchumi wanaosema umelemazwa zaidi na nyongeza kubwa ya ushuru ukiwemo ule wa bei ya mafuta ambao umefanya bidhaa nyingi za kimsingi kupanda mara dufu.

Mengi zaidi kadiri yanavyojiri…

  • Tags

You can share this post!

DONDOO: Barobaro akemea ‘mumama’ aliyejaribu...

Kiptum alenga kukamilisha Rotterdam Marathon kwa muda chini...

T L