• Nairobi
  • Last Updated May 24th, 2024 11:56 AM
Babu Owino: Wakenya wakombolewe kutoka kwa minyororo ya ushuru kupita kiasi

Babu Owino: Wakenya wakombolewe kutoka kwa minyororo ya ushuru kupita kiasi

NA SAMMY WAWERU

MIAKA 60 baada ya Kenya kupata uhuru wa ndani kwa ndani kujitawala, wananchi wanapaswa kukombolewa kutoka kwa minyoror ya ushuru kupita kiasi.

Mbunge wa Embakasi Mashariki, Paul Ongili Owino maarufu kama Babu Owino, amesema ni kinaya Kenya kudai kupata uhuru wa kujitawala ilhali wananchi wangali mateka wa gharama ya juu ya maisha.

Huku bunge likitarajiwa kugaragaza mjadala wa Mswada wa Fedha 2023, mbunge huyo wa ODM, amesema Wakenya wanapaswa kuwa huru kujiendeleza kimaisha badala ya kuwekelewa mzigo mzito wa ushuru.

“Wakenya wanapaswa kuwa huru dhidi ya ushuru unaowaumiza kama vile Kenya ilipata uhuru kutoka kwa mkoloni,” akasema mbunge huyo.

Kauli ya Babu Owino inajiri wakati ambapo wabunge wenzake upinzani wameapa kuzima kupitishwa kwa Mswada wa Fedha 2023.

Ukipitishwa, masuala yaliyopendekezwa yatajumuishwa kwenye Makadirio ya Bajeti 2023/24 yanayotarajiwa kusomwa na Waziri wa Fedha Prof Njuguna Ndung’u Juni 2023.

Mswada huo tata, unapendekeza nyongeza ya ushuru (VAT) wa mafuta ya petroli, kutoka asilimia 8 ya sasa hadi 16.

Nyongeza hiyo inaashiria mfumko wa gharama ya maisha, ikizingatiwa kuwa mafuta na bidhaa za petroli ndizo mizani ya kupanda kwa uchumi.

Serikali ya Kenya Kwanza, Rais William Ruto anashinikiza kupitishwa kwa mswada huo ambao umeonekana kupingwa na Wakenya wengi.

Kando na nyongeza ya VAT ya petroli, unapendekeza kukatwa kwa asilimia tatu ya mishahara ya wafanyakazi fedha hizo Dkt Ruto akidai zitasaidia kufanikisha mpango wa nyumba za bei nafuu.

“Juni 1, 1963 Kenya ilipata uhuru wa ndani kwa ndani kujitawala, tunataka uhuru wa sisi kujitawala kutoka kwa serikali ya Kenya Kwanza,” Babu Owino akasema.

Kinara wa muungano wa upinzani, Azimio la Umoja, Raila Odinga aliye pia kiongozi wa ODM, amepinga kupitishwa kwa mswada huo tata.

Bw Odinga alisema atashawishi wabunge wake kuunganisha bungeni.

  • Tags

You can share this post!

Wandayi: Tutavuruga usomaji bajeti

Wahalifu Mlima Elgon kuona cha mtema kuni

T L