• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 6:55 AM
Baraza la kusimamia biashara ya vyuma chakavu laonya waharibifu wa miundomsingi

Baraza la kusimamia biashara ya vyuma chakavu laonya waharibifu wa miundomsingi

NA CHARLES WASONGA

BARAZA la Kusimamia Biashara ya Vyuma Kuukuu (SMC) limetoa onyo kwa wadau wote katika sekta hiyo wanaoharibu miundomsingi ya umma na ile ya kibinafsi.

Mwenyekiti wa baraza hilo Francis Mugo, amesema baraza hilo limekerwa na ripoti za ongezeko la visa vya wizi wa nyaya na vyuma vilivyotumika kujenga miundomsingi.

Kwenye taarifa aliyoituma  kwa vyombo vya habari mnamo Mei 19, 2023 mwenyekiti huyo alisema wafanyabiashara wa vyuma kuukuu watakaopatikana wakitekeleza uharibifu huo wataadhibiwa kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti Sekta hiyo ya 2015.

“Tayari tumefutilia mbali leseni ya kampuni ya Triple Seven Collectors Ltd mara moja,” Bw Mugo akafichua.

“Vile vile, nawaonya wale ambao huendesha biashara ya vyuma kuukuu bila leseni kutoka baraza hili kwamba wanakabiliwa na hatari ya kukamatwa na biashara zao kufungwa huku wakishtakiwa,” akaongeza.

Mwenyekiti huyo alisema baraza hilo linashauriana na Inspekta Jenerali wa Polisi na Mamlaka ya Ushuru Nchini (KRA) kukusanya habari kuhusu visa vyote vya ukiukaji wa sheria kote nchini, ili hatua hitajika ichukuliwe.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: FKF ichunguze malalamiko yanayoibuliwa kuhusu...

Chiloba awatahadharisha Wakenya wasipokee simu kiholela

T L