• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 1:47 PM
Bei ya mafuta yapaa juu zaidi

Bei ya mafuta yapaa juu zaidi

NA CHARLES WASONGA

NAIROBI, KENYA

MAISHA yataendelea kuwa magumu zaidi nchini baada ya bei ya bidhaa za petroli kupanda kwa kiwango kikubwa zaidi katika historia ya taifa hili.

Bei ya petroli imepanda kwa Sh16.9 kwa lita. Nayo dizeli imeenda juu kwa Sh21.31 huku bei  ya mafuta taa ikipaa kwa Sh33.32 kwa lita moja.

Hii ina maana kuwa petroli itaanza kuuzwa kwa Sh211.64 kwa lita jijini Nairobi huku dizeli ikiuzwa kwa Sh200.9 kwa lita nayo mafuta taa yakiuzwa kwa Sh202.6 kwa lita kuanzia Septemba 14 usiku wa manane.

Hii ni kulingana na bei mpya ambayo imetangazwa hivi punde na Mamlaka ya Kusimamia Sekta ya Kawi na Petroli (EPRA).

Hii ina maana kuwa magari ya uchukuzi ya umma yatapandisha nauli. Aidha, viwanda pia vitaongeza bei za bidhaa ili kufidia gharama ya uzalishaji.

Mazao ya shambani pia yatapanda bei kufidia gharama ya kilimo na uchukuzi.

Kwa ujumla, gharama ya maisha itawasukuma Wakenya kona mbaya kuliko hali ilivyo sasa.

  • Tags

You can share this post!

Huyu anataka tupime ilhali niliokuwa nao walichovya bila...

Vifaabebe kwa watoto wachanga huwacheleweshea uwezo wa...

T L