• Nairobi
  • Last Updated November 28th, 2023 7:53 PM
Bei za mafuta, umeme kupanda tena mswada mpya ukipitishwa

Bei za mafuta, umeme kupanda tena mswada mpya ukipitishwa

NA BRIAN AMBANI

BEI za mafuta na umeme zitaongezeka tena kutokana na mabadiliko yanayopendekezwa kufanyiwa sheria ili kuongeza maradufu ada inayotozwa bidhaa hizo kusaidia kudhibiti sekta hiyo.

Mswada wa kubadilisha Sheria wa 2023 unapendekeza kufanyia mabadiliko Sheria ya Nishati ya 2019 kwa kuongeza ada za EPRA hadi asilimia moja kutoka kiwango cha juu cha sasa cha asilimia 0.5. Wakenya kwa sasa wanalipa Sh0.25 kwa lita ya petroli, dizeli na mafuta ya taa.

Pia wanalipa Sh0.08 kwa umeme kama ada ya Epra.

Ada hizo mbili ni uti wa mgongo wa mapato ya kila mwaka ya mamlaka hiyo. Katika mwaka wa fedha uliokamilika Juni 2021 kwa mfano, Epra iliingiza Sh1.2 bilioni kutoka kwa ushuru wa petroli ikilinganishwa na Sh1.1 bilioni za 2022, ongezeko la asilimia 16.5.

Pia ilipata Sh236 milioni kutokana na ushuru wa umeme katika kipindi hicho, chini ya asilimia 10 kutoka Sh263 milioni mwaka uliopita.

Katika mwaka huo wa fedha, Epra ilipata mapato ya jumla ya Sh1.51 bilioni, ikimaanisha kuwa ada hizo mbili ziliipa hadi Sh1.45 bilioni ikiwa ni sawa na asilimia 96 ya mapato yake.

  • Tags

You can share this post!

Viongozi kutoka Kisii wadai Ruto huenda jimbo lao kuhubiri...

El Nino yaangamiza watu 4 Wajir mafuriko yakilemea kaunti...

T L