• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 2:11 PM
Diwani ajeruhiwa kwenye shambulio la Al-Shabaab Lamu

Diwani ajeruhiwa kwenye shambulio la Al-Shabaab Lamu

NA KALUME KAZUNGU

WATU kadhaa, akiwemo diwani wa wadi ya Hindi Bw James Njaaga na mkewe, wamejeruhiwa baada ya magari kumiminiwa risasi za rasharasha na watu wanaoshukiwa ni wapiganaji wa Al-Shabaab katika eneo la Mwembe, mita chache tu kutoka Lango la Simba katika barabara ya Lamu-Witu-Garsen mnamo Jumanne.

Naibu Kamishna wa Lamu Magharibi Gabriel Kioni amethibitisha kutokea kwa shambulio hilo akisema watu hao waliokuwa na silaha nzito wametekeleza shambulio hilo saa moja na nusu asubuhi.

Walijificha katika pande zote mbili na kufyatua risasi kiholela wakilenga magari yaliyokuwa yakipita katika barabara hiyo, likiwemo gari la diwani huyo.

  • Tags

You can share this post!

CHARLES WASONGA: Mpishi wa Shule ya Mukumu hakustahili...

Ruto awaonya mawaziri wazembe, wafisadi

T L