• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 8:27 PM
DPP Haji apinga kufunguliwa kwa akaunti 30 za Pasta Odero, mawakili wake wakidai serikali inanyanyasa Wakristo

DPP Haji apinga kufunguliwa kwa akaunti 30 za Pasta Odero, mawakili wake wakidai serikali inanyanyasa Wakristo

Na RICHARD MUNGUTI

MCHUNGAJI Ezekiel Odero amepata pigo baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji kupinga vikali kufunguliwa kwa akaunti 30 za kanisa la pasta huyo.

Kutokana na msimamo mkali wa DPP Haji, kupitia mawakili wake amelalamika akidai serikali inawatesa na kuwanyanyasa Wakristo.

DPP aliomba hakimu mkazi Mahakama ya Milimani Ben Mark Ekhubi atupilie mbali ombi la Pasta Odero la kuruhusiwa kuchukua Sh50 milioni za kugharamia mahitaji ya wanafunzi 3, 000 na waumini wa kanisa la New Life Prayer Center and Church (NLPCC).

Kupitia kwa viongozi wa mashtaka James Gachoka na Virginia Kariuki, DPP alisema Bw Ekhubi hana mamlaka ya kutathmini upya na kubatilisha maagizo aliyotoa Mei 8, 2023 akiruhusu mkurugenzi wa uchunguzi wa jina (DCI) kuchunguza chanzo cha mabilioni ya pesa za Mchungaji Odero.

Kiongozi wa mashtaka James Gachoka (kushoto amesimama). Picha / Richard Munguti

“Ikiwa Pasta Odero hajaridhika na maagizo ya hii mahakama ya kufungwa kwa akaunti zake anaweza tu kuililia Mahakama Kuu,” Gachoka alisema.

Bw Gachoka alimsihi hakimu asipotoshwe na madai ya wakili Danstan Omari kwamba kufungwa kwa akaunti za kanisa hilo la NLPCC zichunguzwe ni “kuwatesa Wakristo.”

Bw Gachoka alisema, “Ni Mahakama Kuu peke yake iliyo na mamlaka ya kubatilisha agizo la korti.”

Bw Ekhubi ataamua leo (Alhamisi Mei 18, 2023 ikiwa ataruhusu ombi la Pasta Odero la kufunguliwa kwa akaunti 30.

  • Tags

You can share this post!

Mashambulio makali nchini Sudan mahitaji ya chakula...

Gachagua: Raila apige tu picha na Rais, hakuna kuingia...

T L