• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 1:05 PM
EACC yakataa kumrudishia Oparanya Sh2m ikisema inazipiga darubini

EACC yakataa kumrudishia Oparanya Sh2m ikisema inazipiga darubini

NA RICHARD MUNGUTI

TUME ya Maadili na Kupambana na Ufisadi nchini (EACC), imekataa kumrudishia aliyekuwa Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya Sh2 milioni zilizotwaliwa kutoka kwa makazi yake.

Wakili Philip Kagucia alieleza mahakama ya kuamua kesi za ufisadi nchini kwamba EACC inachunguza chanzo cha pesa hizo kabla ya kuamua ikiwa Oparanya atarudishiwa au la.

Hakimu mkuu mahakama ya kuamua kesi za ufisadi Milimani, Nairobi Thomas Nzyoki, alielezwa na EACC  kwamba inamchunguza Oparanya kwa ubadhirifu wa Sh1.3 bilioni alipokuwa Gavana wa Kakamega.

“Ijapokuwa Oparanya anasema pesa hizo ni kidogo, sio vile. Hizi pesa ni nyingi kwa umma na lazima tubaini Oparanya alizitoa wapi,” alisema Kagucia.

Wakili Davis Osiemo anayemwakilisha Oparanya aliomba mahakama iamuru EACC imrudishie pesa hizo akisema “hazikuwa miongoni mwa hati ambazo zilitakiwa kupigwa darubini.”

  • Tags

You can share this post!

Watu 23 waangamia katika ajali tofauti barabara ya...

Mtundu Sasha Obama apigwa picha akivuta bangi

T L