• Nairobi
  • Last Updated October 2nd, 2023 7:00 AM
Gachagua – Nilikuwa mlevi kabla kuokoka

Gachagua – Nilikuwa mlevi kabla kuokoka

Na WANGU KANURI

NAIBU Rais Rigathi Gachagua amefunguka kuhusu maisha yake ya hapo awali huku akieleza azma yake katika kupigana na pombe.

Akizungumza katika mkutano na washikadau ili kumaliza pombe na matumizi ya dawa za kulevya katika Kaunti ya Nakuru, Bw Gachagua alisema kuwa yeye aliwacha kubugia pombe baada ya kuokoka.

“Rais, Waziri wa Usalama wa Ndani Profesa Kithure Kindiki na wengine wengi hawajawahi kuwa na shida na pombe. Nitakiri kuwa nilikuwa nakunywa pombe sana kabla sijaokoka na wakati nilipoacha, mambo yangu yamekuwa yakinyooka,” akaeleza.

Akiwashawishi waliozama kwenye ulevi kuwacha, Bw Gachagua aliongeza, “Nilipowacha nilijikuza na ndivyo nilikuwa naibu rais. Kwa hivyo nawarai kufikiria pia kuwacha ili mambo yenu yabadilike.”

Huku misako ikiendelea, naibu rais aliwaonya maafisa wa usalama kwa kuchangia kudorora kwa oparesheni hiyo. Aliwalaumu kwa kuendelea kuchukua hongo huku maeneo ya upikaji pombe haramu yakiendeleza biashara hiyo.

“Tunashukuru kuwa polisi wanafanya kazi nzuri lakini wengine wao wamefungua baa zao hivyo kutotekeleza wajibu wao ipasavyo. Ninatashwishi na wale pia wanaochukua hongo, na maafisa wanaopaswa kuwashika walevi lakini wao wamelewa zaidi.”

Kiongozi huyo alisimulia kuwa vijana wengi haswa walio na umri wa miaka 24-35 ndio wameathirika sana na pombe jambo lililochangia kuanzisha msako wao.

Kaunti ya Nyeri ilikuwa ya kwanza oparesheni hiyo kuanzishwa, kufuatia kulemewa na kero ya pombe hasa ile haramu na hatari.

  • Tags

You can share this post!

Ezekiel Mutua: Mchungaji wako si babako au mamako, komeni...

Gachagua adai Uhuru Kenyatta alifumbia macho pombe haramu...

T L