• Nairobi
  • Last Updated February 23rd, 2024 12:15 PM
Ikulu kukosa stima siku nzima – Kenya Power

Ikulu kukosa stima siku nzima – Kenya Power

Na WANGU KANURI

SHIRIKA la Umeme, Kenya Power lilitangaza kuwa hakutokuwa na stima Ikulu ya Rais kutoka saa tatu hadi saa kumi na moja jioni Ijumaa, Mei 26, 2023.

Katika kaunti ya Kiambu, maeneo ya ACME, Njiku, Ombi Rubber, Gatuikira na Maramba pia hayatakuwa na nguvu za umeme.

Kenya Power pia ilisema kuwa kaunti ya Makueni, maeneo yaliyo kwenye barabara ya Mombasa, Nunguni, Kalimbini, Ngokomi, Kwothithu, Kiongwani, Kima, Kiu, Salama, Kautandini, Malili, Enzai, Kilungu na Kavatanzou watasalia kwenye giza.

Maeneo mbalimbali katika kaunti ya Kakamega pia yatasalia bila stima kwa saa nane Ijumaa.

Maeneo hayo ni pamoja na Bukhakhunga, Lukume, Shihome, Power Spot Fact, Bushili, Shikoti, Bukhulunya, The Metrological site na Lurambi pamoja na maeneo yanayozingira sehemu hizo.

Alhamisi, 25 Mei 2023, hakukuwepo na stima kwenye maeneo mengi kaunti ya Nairobi pamoja na kaunti zingine sita. Wakazi wa kaunti za, Homabay, Uasin Gishu, Vihiga, Makueni, Migori na Kiambu hawakuwa na stima kwa saa nane za siku hiyo.

  • Tags

You can share this post!

Sumu kali ndani ya Mswada wa Fedha

Wafuasi wa Maina Njenga wazushia DCI

T L