• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 11:55 AM
Kamati teule yaambiwa Mackenzie alitumia genge kuua wafuasi ‘waliojikokota’ kufa

Kamati teule yaambiwa Mackenzie alitumia genge kuua wafuasi ‘waliojikokota’ kufa

NA NDUBI MOTURI

MHUBIRI Paul Mackenzie alitumia genge la wahalifu kuua wafuasi ‘waliokataa’ kufa hata baada ya kufunga kwa siku nyingi.

Waziri wa Usalama wa Ndani Prof Kithure Kindiki amefichua Ijumaa kuwa genge hilo liliua kwa vifaa butu wafuasi wa Mackenzie ‘waliojikokota’ kufa baada ya kufunga kwa siku kadhaa na wale waliojaribu kutoroka.

Waziri Kindiki ameambia kamati teule ya Seneti inayochunguza vifo vya halaiki katika msitu wa Shakahola, Kaunti ya Kilifi, kuwa Mackenzie alitumia mbinu mbalimbali kuficha mauaji hayo.

“Alikuwa akitapeli wafuasi wake fedha lakini alipendelea kupewa hela taslimu badala ya kutumiwa kwa simu,” amesema.

Mackenzie anadaiwa kutumia kanisa lake la Good News International kushawishi wafuasi wake kuuza mali za na kisha kujiunga na kanisa.

Baadaye, aliwahadaa akiwashawishi kutokula au kunywa hadi wafe ili wakutane na Yesu.

Waliobadili nia na kutaka warudishwe nyumbani waliuawa na genge hilo, Prof Kindiki ameambia maseneta.

“Baadhi ya makaburi ya waathiriwa yalifunikwa kwa nyasi na ndiyo maana maafisa wetu wamekuwa na kibarua kigumu kuyatafuta,” akasema.

Kufikia sasa, miili ya watu 241 imefukuliwa kutoka katika kipande cha ardhi ya ekari 800 inayoaminika kumilikiwa na Mackenzie.

Watu zaidi ya 90 wameokolewa kutoka msituni humo kufikia sasa.

  • Tags

You can share this post!

Gaspo Women wapiga abautani na kuamua kucheza dhidi ya...

Kunipigia kura haikumaanisha mkatalie na Hasla Fund,...

T L