• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 1:29 PM
Karua amshambulia Ruto kuhusu ushuru

Karua amshambulia Ruto kuhusu ushuru

Na WANGU KANURI

MARTHA Karua alimshambulia Rais William Ruto wakati wa Kongamano la Kitaifa la Jubilee, kuhusu pendekezo la kutoza na kuongeza ushuru (VAT).

Akimwita Zakayo mtoza ushuru, kama Zakayo wa Biblia, Bi Karua alimwonya kuwa asiposhukisha ushuru basi Wakenya watamshukisha.

Kwa maneno makali, Bi Karua aliwafananisha wakuu katika serikali ya Rais Ruto kama watu waonevu huku akisema kuwa watasimamia haki zao.

“Mambo ya ushuru wewe Zakayo utashusha na usiposhuka Wakenya watakushukisha,” akasema.

Bi Karua pamoja na viongozi wengine wa muungano wa Azimio la Umoja – One Kenya wamemshutumu sana Dkt Ruto kwa gharama ya juu ya maisha.

Hivi majuzi, serikali iliongeza bei ya mafuta taa kwa Sh15.19 baada ya kuondoa ruzuku ya bidhaa hiyo, na kufanya bei yake kupanda kwa asilimia 9.4.

Kuanzia Mei 15 hadi Juni 14 bei ya mafuta taa iliongezeka hadi Sh161.13 kwa lita jijini Nairobi kwa mujibu wa Mamlaka ya Kuthibiti Kawi na Petroli (Epra).

Mamlaka hiyo pia iliongeza bei ya dizeli kwa asilimia 3.9 hadi Sh168.4 kwa lita jijini Nairobi.

Huku mafuta na petroli yakiwa kisaidia kwa asilimia kubwa uendeshaji wa biashara na nchi kwa ujumla, bei ya bidhaa ilianza kuongezeka.

Sukari ya pakiti mbili kwa mfano inanunuliwa kwa Sh400.

Nauli imeongezeka, unga, chumvi, na hata mafuta havinunuliki kwa bei ya hapo awali.

  • Tags

You can share this post!

Uhuru Kenyatta: Sitishiki licha ya kondoo wangu kuibwa

Raila: Uhuru ni shujaa kwa kuhepa vitisho na kuandaa mkutano

T L