• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 1:05 PM
Katibu Esther Ngero ajiuzulu kazi serikalini

Katibu Esther Ngero ajiuzulu kazi serikalini

NA MWANDISHI WETU

KATIBU wa Idara ya Huduma za Urekebishaji Tabia Esther Ngero amejiuzulu kwa sababu za kibinafisi wiki moja tu baada ya Rais William Ruto kumhamisha kutoka kwa Idara ya Kusimamia Utendakazi na Utoaji Huduma katika Ofisi ya Mkuu wa Mawaziri.

Idara ya Huduma za Urekebishaji Tabia iko katika Wizara ya Usalama wa Ndani inayoongozwa na Waziri Prof Kithure Kindiki.

“Mheshimiwa Rais amepokea barua ya kujiuzulu kwa Bi Esther Ngero na kukubali japo shingo upande, ikizingatiwa kwamba mtumishi huyo wa umma ametaja sababu za kibinafsi,” amesema Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei.

Kabla ya kuingia serikalini akiwa Katibu mnamo Desemba 2022 baada ya kuteuliwa, Bi Ngeru alikuwa akifanya kazi katika sekta ya mafuta kwa miongo miwili.

  • Tags

You can share this post!

Wazee wa Kaya wadai kumiliki shamba la Mackenzie

Dadake Betty Kyalo aajiri mtunzi wa watoto wa mbwa wake

T L