• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 11:30 AM
KCPE 2023: Wasiwasi matokeo ya mtihani yakikawia kutumwa kieletroniki 

KCPE 2023: Wasiwasi matokeo ya mtihani yakikawia kutumwa kieletroniki 

NA SAMMY WAWERU

HALI ya taharuki imekumba watahiniwa wa Mtihani wa Kitaifa Darasa la Nane (KCPE) 2023, walimu na wazazi kufuatia kukawia kwa matokeo kwa njia ya kieletroniki.

Baada ya Waziri wa Elimu kutoa rasmi matokeo hayo, Alhamisi, Novemba 23, 2023 katika makao makuu ya mitihani, Mitihani House, Jijini Nairobi, ili kuyapokea upesi watahiniwa wametakiwa kutuma ujumbe mfupi wa nambari zao za kuandika mtihani (INDEXNUMBER) kwa nmabari 40054.

Ujumbe huo aidha unatumwa kwa simu ya mkono.

Nambari hizo, hata hivyo, zinakawisha matokeo walimu, wanafunzi na wazazi wakihimiza serikali kuangazia tatizo hilo.

Saa moja baada ya matokeo hayo kutangazwa rasmi, hakukuwa na mtahiniwa kote nchini aliyekuwa amejua alama alizopata.

“Mteja mpendwa, matokeo ya KCPE 2023 hayapo kwa sasa. Tafadhali jaribu tena baadaye. Nambari ya usaidizi ya KNEC ni 08007224900,” ilisema sehemu ya ujumbe kwenye simu ya mzazi mmoja Mombasa aliyetuma ujumbe akitafuta matokeo.

Mtahiniwa bora zaidi amezoa alama 428, kwa jumla ya 500 zinazowezekana.

Jumla ya watahiniwa 1, 406, 559 walifanya KCPE 2023, wa kiume wakiwa 721, 544 na kike 685, 017.

Hadi wakati wa kuchapisha taarifa hii, hitilafu hiyo ya kimitambo haikuwa imetatuliwa.

Soma pia: https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kitaifa/michael-warutere-mtahiniwa-aliyezoa-alama-428-katika-kcpe-2023-anataka-kuwa-mhandisi

  • Tags

You can share this post!

Mchecheto wagubika wazazi, watahiniwa hitilafu ya mitambo...

KCPE: Mtahiniwa bora 2023 aandikisha punguo la alama 3...

T L