• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 5:22 PM
Madaraka Dei 2023: Rangi maridadi za vikosi vya pamoja vya usalama gwarideni

Madaraka Dei 2023: Rangi maridadi za vikosi vya pamoja vya usalama gwarideni

 

NA SAMMY WAWERU

RAIS William Ruto anaongoza taifa Alhamisi kuadhimisha Madaraka Dei, Juni 1, 2023.  

Ni siku Kuu ambapo Kenya huiadhimisha kila mwaka, kukumbuka siku ambayo ilipata uhuru wa ndani kwa ndani kujitawala kutoka kwa serikali ya Mbeberu 1963.

Maadhimisho haya yanafanyika katika Uwanja wa Moi, Kaunti ya Embu.

Vikosi vya pamoja vya usalama, vinatarajiwa kuandaa gwaride la heshima mbele ya Rais Ruto huku maafisa husika wakiwa wamevalia sare zao rasmi.

Vinajumuisha kikosi cha majeshi ya Kenya (KDF), Kikosi cha askari wa kawaida (Kenya Police), askari tawala (AP), maafis wa kukabiliana na ghasia (GSU), misitu (KFS), Wanyamapori (KWS) na Shirika la Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS).

Mpiga picha wetu, Joseph Kanyi amenasa picha za kipekee maafisa hao wakifanya mazoezi na kujiandaa kupamba Madaraka Dei 2023.

Vikosi vya pamoja vya usalama vikifanya mazoezi kwa minajili ya gwaride la heshima, maadhimisho ya Madaraka Dei, Juni 1, 2023. Picha zote / JOSEPH KANYI
  • Tags

You can share this post!

Moraa aamua kushiriki riadha za polisi badala ya Diamond...

Vituko: Sonko athibitisha ‘blingi’ zake si feki

T L