• Nairobi
  • Last Updated October 2nd, 2023 7:00 AM
Mahakama yaidhinisha wakili Mitchell Kemuma kuwa MCA maalum Nyamira

Mahakama yaidhinisha wakili Mitchell Kemuma kuwa MCA maalum Nyamira

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA Kuu imeidhinisha uteuzi wa wakili Mitchell Kemuma kuwa Diwani maalum (MCA) katika Kaunti ya Nyamira, kwa tikiti ya chama cha Jubilee.

Jaji Lucy Mwihaki Njuguna alifutilia mbali uteuzi wa Bi Dolphine Nyang’ara ambaye ni mkazi wa Kaunti Kiambu alikojiandikisha kama mpiga kura.

Katika uamuzi wak, Jaji Njuguna alisema jina la Bi Nyang’ara ambaye amekula mishahara kwa miezi tisa sasa kinyume cha sheria liliwasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) na mwenyekiti wa chama cha Jubilee.

Alisema pia Jubilee kupitia Katibu wake Mkuu Jeremiah Kioni iliwasilisha orodha nyingine, kisha IEBC ikamteua Bi Nyang’ara kinyume cha sheria.

Wakili Kemuma alipinga uteuzi wa Bi Nyang’ara katika mahakama ya Nyamira.

Mahakama ya Nyamira ilifutilia mbali uteuzi wa Bi Nyang’ara ambaye alikata rufaa katika jopo la kuamua mizozo ya vyama vya kisiasa (PPDT) ambapo pia iliratibisha uteuzi wa Bi Kemuma.

Bi Nyang’ara alikataa rufaa tena katika mahakama ambapo uteuzi wake ulifutiliwa mbali.

“Baada ya kutathmini ushahidi wote uliowasilishwa katika rufaa hii nimefikia uamuzi Bi Kemuma ndiye angeteuliwa kuwa diwani maalum badala ya Bi Nyang’ara ambaye amejiandikisha kuwa mpiga kura katika Kaunti ya Kiambu eneo la Mlima Kenya,” aliamuru Jaji Njuguna.

Jaji huyo aliamuru nakala ya uamuzi wake wa uteuzi wa Bi Kemuma uwasilishwe kwa IEBC na chama cha Jubilee, jina lake lichapishwe katika Gazeti Rasmi la Serikali.

Jaji Njuguna aliagiza kitita cha Sh200, 000 kilichowekwa kama dhamana ya gharama ya kesi na Bi Nyang’ara arudishiwe.

Jina la Nyang’ara aliyepinga kesi ya kutimuliwa kuwa diwani maalum alisema aliteuliwa na IEBC na hakufanya makosa yoyote anyang’anywe kiti.

Chama cha Jubilee (JPK) kilimteua Septemba 9, 2022.

Lakini Ndubi Mokua aliyemwakilisha Bi Kemuma alimweleza Jaji Njuguna kwamba uteuzi wa Bi Kemuma uliambatana na agizo la jopo la kuamua mizozo ya vyama vya kisiasa (PPDT).

Jaji Njuguna alielezwa JPK ilibadilishe orodha ya majina iliyowasilisha kwa IEBC ya kuteuliwa kuwa diwani maalum.

Jaji Mwihaki alifahamishwa katibu mkuu wa JPK aliandikia IEBC akiomba majina yabadilishwe kwa mujibu wa uamuzi wa PPDT lakini haikutekeleza agizo la PPDT.

Bw Mokua alisema kufuatia uamuzi wa PDT Bi Kemuma aliteuliwa.

Pia wakili huyo alitetea uamuzi wa mahakama ya Nyamira ukiratibisha uteuzi wa Bi Kemuma.

Lakini wakili Wilkins Ochoki alisema hakimu mkazi William Chepseba alikosea kuratibisha uteuzi wa Bi Kemuma.

Bw Ochoki alisema kubadilishwa kwa orodha ya uteuzi wa madiwani maalum na JPK ulikinzana na sheria za uchaguzi.

  • Tags

You can share this post!

Machifu na wakuu wa askari watakaoshindwa kuzima pombe...

Maina Njenga aachiliwa kwa dhamana wakili wake akidai...

T L