• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Maina Njenga afikishwa mahakamani akidaiwa kuhusika na vitendo vya uhalifu

Maina Njenga afikishwa mahakamani akidaiwa kuhusika na vitendo vya uhalifu

NA JOSEPH OPENDA

ALIYEKUWA kiongozi wa kundi lililopigwa marafuku la Mungiki, Maina Njenga amefikishwa katika Mahakama ya Nakuru leo Jumatano asubuhi.

Anatarajiwa kusomewa mashtaka kadhaa yakiwemo yale ya kuwa mwanachama wa kundi haramu na kujihusisha na vitendo vya uhalifu uliopangwa.

Maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wamekuwa wakimwinda Njenga baada ya bastola mbili na misokoto ya bangi kupatikana katika makazi yanayodaiwa kuwa yake katika eneo la Wanyororo jijini Nakuru.

Kwenye operesheni, maafisa walikamata watu wanane.

“Aliyekuwa kiongozozi wa Mungiki anatafutwa ili ahojiwe baada ya bangi na bunduki kupatikana katika boma linalodaiwa kuwa lake. Aliye na habari za aliko kiongozi huyo wa zamani wa Mungiki, ambaye tayari yuko mafichoni, aziwasilishe kwa DCI,” DCI ikasema kwenye taarifa iliyochapisha kwa ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.

Majuzi Njenga alionekana kwenye mazishi ya Mama Mukami Kimathi ambaye hadi kifo chake alikuwa mjane wa mpiganiaji uhuru Shujaa Dedan Kimathi.

  • Tags

You can share this post!

Mandonga ‘Mtu Kazi’ kusisimua tena Nairobi

Rais wa Tanzania ajitokeza kusaidia Yanga kwa hali na mali

T L