• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 11:55 AM
Makundi ya kidini Kenya yasifu Rais Museveni kuharamisha ushoga na usagaji

Makundi ya kidini Kenya yasifu Rais Museveni kuharamisha ushoga na usagaji

NA TITUS OMINDE
SIKU moja baada ya Rais wa Uganda Yoweri Museven kutia saini sheria kuharamisha ushoga na usagaji nchini, Baraza Kuu la Wasomi wa dini ya Kiislamu nchini maarufu FATWA limeunga mkono hatua hiyo.

Naibu mwenyekiti wa baraza hilo Sheikh Abubakar Bini alipongeza Rais Museveni huku akitaka viongozi wengine barani Afrika kuiga mfano wa Bw Museveni.

“Kama mwenyekiti wa baraza la FATWA naunga mkono Rais Museveni kwa hatua hiyo. Viongozi wa bara nzima la Afrika hawana budi ila kuunga mkono hatua ya Rais Museveni,” alisema Sheikh Bini.

Sheikh Bini alitoa changamoto kwa bunge la Kenya kuanzisha mchakato kuwasilsisha mswada sawia bungeni ili kufwata nyayo za rais wa Uganda.
Akihutubu mjini Eldoret, Sheikh Bini alitaka viongozi wa humu nchini kutohofia vitisho vya mataifa ya Magharibi kuwanyima misaada kwa kutia saini mswada kama huo na kuwa sheria.

Kiongozi huyo wa kidini alisema ni heri kukwepa laana ya Mwenyezi Mungu na kukosa chakula cha kimwili badala ya kukubali unajisi unaotokana na ushoga.

Kwa sasa anataka Rais William Ruto kuwa tayari kuunga mswada huo, akisema iwapo wabunge watasita kuwasilisha mswada sawa na Uganda bungeni, wasomi wa dini ya Kiislamu wameanza harakati kuuwasilisha bungeni kwa niaba ya Wakenya wapenda maadili.

“Natoa wito kwa Rais William Ruto kuonyesha ukakamavu wake kama mkristo mpenda utu na Uungu kuiga mfano wa kiongozi wa Uganda na kutia saini kuwa sheria mswada huo baada ya kuwasilishwa katika bunge la humu nchin,” alisema Sheikh Bini.

Kwa mujibu wa Sheikh Bini ni kwamba mswada huo utampa Rais wa Uganda umaarufu barani Afrika na kutambulika kama shujaa aliyepuuza vitisho vya mataifa ya Magharibi na kuweka mbele maadili ya Kiafrika.

Msimamo sawa ulitolewa na baraza la wahubiri na Maimam nchini ambao walisema watatumia kila mbinu kuona kuwa nch ya Kenya imebuni sheria kuzima ushoga na usagaji.

Vile vile, Askofu Peter Simwa ambaye ni mwenyekiti wa muungano wa wahudumu wa Injili mjini Eldoret ameunga mkono hatua ya Rais Museveni huku akisema kuwa LGBTQ ni kinyume na mafunzo ya Bibilia ambapo tabia hiyo inadhalilisha maadili.

“Bibilia haiungi mkono ushoga, natumai serikali yetu itaiga mfano wa rais wa Uganda na kubuni sheria sawa hapa nchini,” alisema askofu Simwa.

Mhubiri huyo alisema hivi karibuni wachungaji watafanya maandamanao mjini humo kushinikisha wabunge kubuni sheria kuharamisha ushoga na usagaji.

Mswada uliotiwa saini na Rais Museveni unapendekeza vifungo vya maisha kwa watakaopatikana wakijihusisha na vitendo vya ushoga na usagaji.

  • Tags

You can share this post!

Delmonte yawapiga jeki wasichana wa Mwana Wikio kwa kuwapa...

Hamasisho lapunguza idadi ya wanaofariki wakijifungua...

T L