• Nairobi
  • Last Updated June 12th, 2024 4:24 PM
Mbunge adai watu mashuhuri Mlima Kenya wamepiga jeki Raila kwa Sh10 bilioni kufanya maandamano

Mbunge adai watu mashuhuri Mlima Kenya wamepiga jeki Raila kwa Sh10 bilioni kufanya maandamano

NA SAMMY WAWERU

MBUNGE wa Thika mjini Alice Ng’ang’a amedai anajua wanaofadhili maandamano ya Azimio kuafikia matakwa yao.

Akitoa onyo, mbunge huyo wa United Democratic Alliance (UDA) alitishia Jumapili kwamba atawaanika.

Alidai kwamba kiongozi wa Azimio, Bw Raila Odinga anafadhiliwa na baadhi watu mashuhuri kutoka jamii ya Mlima Kenya kufanya maandamano.

Kuling’ana na Ng’ang’a, baadhi ya wafadhili wa maandamano yanayotarajiwa kufanyika leo, Jumatatu kwa mara ya pili ni watu walioshikilia nyadhifa kuu serikalini awali.

“Tunajua ulipokea kima cha Sh10 bilioni kuhangaisha serikali kupitia maandamano,” mbunge huyo akadai.

Alisema hayo wakati akihutubu katika kanisa la AIPCA Thika, katika hafla ya shukrani kufuatia uteuzi wa Waziri wa Biashara Bw Moses Kuria.

Mbunge huyo aidha alidai serikali ya Kenya Kwanza, inayoongozwa na Rais William Ruito na naibu wake Rigathi Gachagua ina ushahidi wa Raila Odinga kufadhiliwa kuendeleza maandamano.

“Tuna picha za njama ilivyotekelezwa,” Ng’ang’a akasema.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga akiwa Huruma jijini Nairobi kwenye maandamano ya Jumatatu, Machi 20, 2023. PICHA | DENNIS ONSONGO

Raila ameapa kufanya maandamano leo, licha ya onyo la Inspekta Mkuu wa Polisi, IG Japhet Koome mnamo Jumapili ambapo alitaja maandamano hayo kuwa haramu.

Afisa huyo mkuu akitishia kuadhibu kisheria watakaoshiriki, Bw Odinga alimtaka Koome mwenyewe kumkamata badala ya kutumia askari wake.

Azimio inashinikiza serikali kushusha gharama ya maisha, shughuli ya uteuzi wa makamishna wapya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kusitishwa na makamishna waliojiuzulu na kufurushwa kurejeshwa mara moja.

Hali kadhalika, vuguvugu la upinzani linataka sava ya IEBC kufunguliwa kubaini ukweli wa matokeo ya kura za urais Agosti 9, 2022 licha ya kesi ya Azimio kupinga ushindi wa Rais Ruto kufutiliwa mbali na mahakama ya upeo.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Serikali ifichue mashirika yaliyopigwa marufuku...

Ruto ampa Raila nguvu

T L