• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Mbunge aliyeonyesha chuki kwa Hayati Mzee Jomo Kenyatta afariki

Mbunge aliyeonyesha chuki kwa Hayati Mzee Jomo Kenyatta afariki

Na KITAVI MUTUA na WANGU KANURI

MBUNGE aliyeonyesha hadharani chuki kwa aliyekuwa rais wa kwanza nchini Hayati Mzee Jomo Kenyatta aliaga dunia.

Gedion Mutiso, mbunge wa kwanza katika eneobunge la Yatta, alifariki mapema wiki jana akiwa na miaka 91.

Bw Mutiso alishtua nchi baada ya kukiri kuwa atajihusisha na mapinduzi ya kiserikali ya 1971.

Mbunge huyo ambaye alikuwa akiisuta serikali wakati alikuwa akihudumu alikiri hivyo kortini alipokuwa akishtakiwa kwa kosa la usaliti.

Bw Mutiso alikuwa ametiwa mbaroni mnamo 1971 pamoja na wenzake waliokuwa wakipanga mapinduzi hayo na kushtakiwa kwa kupanga kupindua serikali kwa njia zisizo halali.

Hata hivyo, alipokuwa kizimbani, Bw Mutiso hakuficha chuki yake ya jinsi Mzee Kenyatta alivyoiongoza nchi huku akisema uongozi wake mbaya ndio ulimfanya kupanga njama ya mapinduzi.

Mbunge huyo wa zamani alieleza hakimu S.K. Sachdeva kuwa nyakati nyingi alikuwa na mikutano na Jenerali Joseph Ndolo, aliyekuwa mkuu wa wafanyikazi kujadili mipango ya kupindua serikali ya Mzee Kenyatta.

Jenerali Ndolo alipigwa kalamu baada ya maungamo ya Bw Mutiso. Isitoshe, viongozi wengine wakubwa serikalini pia walijiuzulu ikiwemo aliyekuwa Jaji Mkuu Kitili Mwendwa.

Alipopatikana na hatia na kufungwa gerezani kwa miaka 10, kiti chake kilinyakuliwa na Simon Kitheka Kiilu lakini aliwania tena ubunge baada ya kutoka jelani na kushinda mnamo 1983.

Bw Mutiso alihudumu kama mbunge wa eneo hilo hadi mwaka wa 1997 aliposhindwa. Hata hivyo, miaka yake ilipoendelea, Bw Mutiso aliondoka katika siasa na kuanza ukulima pamoja na kufanya biashara.

Kwa mujibu wa mtoto wake Frank Mutiso, babake aliwachiliwa jelani mnamo 1981 na aliyekuwa rais wa pili marehemu Daniel Moi, miezi mitatu kabla ya kumaliza kifungo chake.

Licha ya kuachiliwa, Bw Mutiso alikatazwa kujumuika na watu na kuamrishwa kukaa nyumbani.

  • Tags

You can share this post!

CHARLES WASONGA: Serikali ifanikishe azma ya afya kwa wote...

Jubilee Party: Mrengo wa Kanini Kega wamng’oa Uhuru

T L