• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 6:50 PM
Mhubiri kutoka Nigeria ashtakiwa kwa kupora benki mamilioni ya pesa

Mhubiri kutoka Nigeria ashtakiwa kwa kupora benki mamilioni ya pesa

Na RICHARD MUNGUTI

PASTA kutoka Nigeria ameshtakiwa kwa kula njama za kuitapeli benki mamilioni ya pesa.

Pasta Wealth Ochelle almaarufu Apostle Wealth wa Kanisa la Cogic International Church of God lililoko eneo la Shanzu, Kaunti ya Mombasa, anakabiliwa na mashtaka kutapeli benki Sh28.7 milioni.

Alipofikishwa mbele ya Hakimu Mkuu Mahakama ya Milimani Nairobi Lucas Onyina, alisomewa mashtaka mawili.

Shtaka la kwanza lilikuwa la kula njama za kuipunja Stanbic Bank Limited Sh28, 779, 600.

Kiongozi wa mashtaka Bw Anderson Gikunda alieleza mahakama mshtakiwa aliashiria kutekeleza uhalifu huo kati Novemba 3 na 8, 2022.

Shtaka lilisema alipanga kuitapeli benki hiyo mahala pasipojulikana humu nchini.

Alikabiliwa na shtaka la pili la kupatikana amehifadhi kitita cha Sh340, 000 mnamo Novemba 10, 2022 akijua pesa hizo zimeibwa au kupatikana kwa njia isiyo halali.

Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh500, 000.

Kesi itatajwa Juni 9, 2023.

 

  • Tags

You can share this post!

Pasta tapeli wa mashamba taabani

Atakayechukua nafasi ya Sabina Chege kutajwa katika PG ya...

T L