• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 6:55 PM
Miguna Miguna aomba wahusika wa sukari ya sumu na Kemsa kufungwa 

Miguna Miguna aomba wahusika wa sukari ya sumu na Kemsa kufungwa 

Na WANGU KANURI

WAKILI Miguna Miguna ameiomba serikali kuwafunga jelani wahusika wakuu wa kuuza sukari ya sumu kwa umma pamoja na wale waliohusika katika sekta ya Shirika la Kusambaza Dawa na Vifaa vya Matibabu Kenya (KEMSA).

Kwenye ujumbe wake, Miguna alisema kuwa wahusika hao hawapaswi kupewa hata mshahara au kuajiriwa kwingine.

Licha ya Rais William Ruto kumfuta kazi Katibu wa Afya ya umma, Dkt Josephine Mburu, Afisa Mkuu Mtendaji wa Kemsa Terry Ramadhani na kuvunja bodi ya Kemsa, Miguna alikiri kuwa pesa zilizokuwa zinanuiwa kuibiwa zinafaa kurudishwa kwa Wakenya.

“Wahalifu hao waliouza sukari yenye sumu kwa umma pamoja na wale walioiba au waliojaribu kuiba mabilioni ya pesa kule Kemsa wanapaswa kukamatwa, kushtakiwa na kufungwa jela na pesa walizoiba au faida walizopokea kutoka kwa sukari hiyo yenye sumu kurudishwa kwa umma pamoja na faida,” akaandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Rais Ruto aliwafuta maafisa hao wa Kemsa sababu ya kashfa ya Sh4 bilioni ya vyandarua vya kujikinga na mbu siku moja baada ya kuonya maafisa wa mashirika ya serikali kwamba utawala wake hautavumilia ufisadi na utepetevu.

Serikali imeanza uchunguzi kuhusu sakata ya sukari ya sumu inayodaiwa kuuziwa Wakenya na wafisadi serikalini.

Magunia 10,000 ya kilo 50 kila moja iliwasili Mombasa kutoka Zimbabwe mnamo Juni 30, 2018 lakini ikatoweka katika hali ya kutatanisha kutoka katika ghala ya Vineyard iliyoko katika eneo la Makongeni mjini Thika.

Rais Ruto tayari amemtimua Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kudhibiti Ubora wa Bidhaa Nchini (Kebs) Bernard Njiraini pamoja na maafisa wengine 26 wa idara mbalimbali za seriklai wamesimamishwa kazi kwa muda kuhusiana na sukari hiyo ya sumu.

Kebs ilikuwa imepiga marufuku matumizi ya sukari hiyo huku ikisema kuwa ilikuwa hatari kwa afya. Sakata hiyo ya sukari ya sumu inaaminika kuuzwa na viongozi wawili wa ngazi ya juu serikalini.

 

  • Tags

You can share this post!

Akothee afichua kuanza kumeza dawa za kusaidia kushika...

Dai wakristo wanateswa na serikali

T L