• Nairobi
  • Last Updated May 30th, 2023 10:25 AM
Mlinzi akiri kuwa na bastola bila leseni

Mlinzi akiri kuwa na bastola bila leseni

Na RICHARD MUNGUTI

MLINZI wa kibinafsi wa mfanyabiashara Chris Philip Okeyo Obure amekiri kortini kwamba hakuwa na leseni ya bastola iliyotumika katika mauaji ya mfanyabiashara Kevin Omwenga.

Robert John Ouko Bodo alimweleza hakimu mwandamizi Bernard Ochoi kwamba bastola aliyokuwa nayo mahakamani ilikuwa ya Obure.

Akihojiwa na kiongozi wa mashtaka James Gachoka, alipojitetea katika kesi ya kupatikana na bastola na risasi bila leseni mnamo Agosti 2, 2000 katika makazi ya Galana Suites Nairobi, Bodo alisema “ijapokuwa nilikuwa natumia bastola ya Obure kumlinda sikuwa na leseni.”

Bodo alifichua, Obure ndiye alikuwa amepewa leseni na asasi ya silaha.

  • Tags

You can share this post!

Mechi ya Harambee Starlets dhidi ya Albania yazama

Washukiwa wa Sagini kung’olewa macho wana kesi ya...

T L