• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Msikiti wa Jamia waandaa siku ya hamasisho, Wakristo wakipata fursa ya kufahamu Uislamu

Msikiti wa Jamia waandaa siku ya hamasisho, Wakristo wakipata fursa ya kufahamu Uislamu

NA CECIL ODONGO

WITO wa umoja miongoni mwa waumini wa dini zote ili kukabili changamoto za nchi ulitawala Siku ya Hamasisho Kuhusu Uislamu katika msikiti wa Jamia jijini Nairobi, mnamo Jumamosi.

Wakati wa hafla hiyo, uongozi wa msikiti huo umewakaribisha Wakenya wa dini zote kutembelea msikiti, kufahamu mengi kuhusu Uislamu kwa kuuliza maswali kisha kupata majibu kutoka kwa wasomi wa dini hiyo.

Abu Sufyan Ahmed awaelekeza wageni wasiokuwa Waislamu ambao wamefika kwa msikiti wa Jamia siku ya Hamasisho kuhusu Uislamu kujifunza mengi kuhusu dini hiyo. PICHA | WILFRED NYANGARESI

Kwa mujibu wa Imam wa Jamia Sheikh Jamaldin Osman wamefungua milango ya msikiti ili kuleta uelewano na kuwezesha wengi kufahamu dini hiyo.

Imam wa Msikiti wa Jamia, Sheikh Jamaludin Osman ahutubia waumini wa dini ya Kiislamu baada ya swala ya adhuhuri katika msikiti wa Jamia jijini Nairobi mnamo Juni 3, 2023. Wasimamizi wa msikiti huo wameandaa Siku ya Hamasisho kuwapa fursa wasiokuwa Waislamu kujifunza mengi kuhusu dini hiyo. PICHA | WILFRED NYANGARESI

Sheikh Osman ametaja ubaguzi, fitina na ukabila akisema ni kati ya mambo ambayo yatatokomezwa iwapo kila dini itafungua milango kwa wale ambao si waumini wake kufahamu yaliyomo.

“Sisi hatulazimishi mtu kuingia Kusilimu lakini binadamu ana hiari kuingia Uislamu. Mimi nina jukumu la kufundisha ukweli kuhusu dini hii badala ya dhana zinazoenzwa si kweli. Wakristo na Waislamu wote wapo katika nchi kwa hivyo heshima na maelewano inapatikana tukitangamana na kufahamiana,” akasema Sheikh Osman.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Daawa (Da’wah) Mohamed Sheikh amesema zaidi ya Wakenya 700 wamejitokeza katika msikiti huo ili kupata mafunzo na kujua mengi kuhusu Uislamu.

Mwislamu atawadha kabla ya kuwahi swala katika Msikiti wa Jamia jijini Nairobi mnamo Juni 3, 2023. Wasimamizi wa msikiti huo wameandaa Siku ya Hamasisho kuwapa fursa wasiokuwa Waislamu kujifunza mengi kuhusu dini hiyo. PICHA | WILFRED NYANGARESI
  • Tags

You can share this post!

Serikali yaonya walimu wanaosisitiza sare zinunuliwe...

Mhubiri Paul Mackenzie awaambia wanahabari wamnunulie...

T L