• Nairobi
  • Last Updated October 2nd, 2023 7:00 AM
Mudavadi ahofia majanga zaidi yatazuka bara Afrika

Mudavadi ahofia majanga zaidi yatazuka bara Afrika

NA MERCY SIMIYU

MKUU wa Mawaziri, Bw Musalia Mudavadi ameelezea hatari inayoikabili Afrika kutokana na majanga yanayosababishwa na binadamu na sababu nyingine za kimaumbile.

Akiongea Jumapili, Septemba 17, 2023 katika Kongamano la Afrika la Shirikisho la mashirika ya Msalaba Mwekundu na Red Crescent (IFRC) jijini Nairobi, Bw Mudavadi alisema majanga haya yanasababisha maafa, watu kupoteza makao na kuvurugwa kwa njia za kuchuma mapato barani Afrika.

Aidha, alisifu kazi nzuri inayofanywa na IFRC katika kusaidia jamii za Kiafrika zinazoathiriwa na majanga haya na mabadiliko ya tabianchi.

“Inasikitisha kuwa Barani Afrika tunaendelea kushuhudia majanga mbalimbali yanayosabishwa na shughuli za binadamu, mabadiliko ya tabianchi na matukio mengine ya kimaumbile,” akasema Bw Mudavadi.

“Ni kinaya kuwa japo Afrika haichangii sana katika uchafuzi wa anga na mazingira, ndiyo inayobebeshwa mzigo wa athari za mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na uchafuzi kama vile mafuriko, ukame na mengineyo,” akaongeza.

  • Tags

You can share this post!

Ukatili: Mwanafunzi wa UoN akifumaniwa akimnajisi dadake  

Utalii Lamu unavyoyumbishwa na mfumko wa bei ya mafuta ya...

T L