• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 4:47 PM
Nauli nazo zapanda

Nauli nazo zapanda

NA KEVIN CHERUIYOT

MUUNGANO wa Wamiliki wa Matatu (MOA) watangaza nauli inapanda kwa asilimia 20 kwa barabara zote nchini.

Akitangaza nauli mpya jijini Nairobi mnamo Ijumaa, mwenyekiti wa MOA Albert Karakacha amesema hatua hii inatokana na kupanda kwa bei ya mafuta.

“Wadau katika sekta ya matatu tumekuwa na majadiliano ya kina, na wamiliki wa matatu wamesema hatua nzuri kuwawezesha kuendelea na biashara ya uchukuzi ni kupandisha nauli,” amesema Bw Karakacha.

Bei ya petroli imepanda kwa Sh16.9 kwa lita. Nayo dizeli imeenda juu kwa Sh21.31 huku bei ya mafuta taa ikipaa kwa Sh33.32 kwa lita moja.

Hii ina maana kuwa petroli itaanza kuuzwa kwa Sh211.64 kwa lita jijini Nairobi huku dizeli ikiuzwa kwa Sh200.9 kwa lita nayo mafuta taa yakiuzwa kwa Sh202.6 kwa lita kuanzia Septemba 14 usiku wa manane.

Bei mpya zilitangazwa na Mamlaka ya Kusimamia Sekta ya Kawi na Petroli (EPRA) mnamo Alhamisi.

Aidha, viwanda pia vitaongeza bei za bidhaa ili kufidia gharama ya uzalishaji.

Mazao ya shambani pia yatapanda bei kufidia gharama ya kilimo na uchukuzi.

Kwa ujumla, gharama ya maisha itawasukuma Wakenya kona mbaya kuliko hali ilivyokuwa kipindi cha mwezi mmoja ambao umepita.

  • Tags

You can share this post!

Bungoma Queens waingia sokoni kusaka majembe kabla ya msimu...

Ndoa zasimama talaka zikipungua nchini, afichua Kadhi Mkuu

T L