• Nairobi
  • Last Updated October 2nd, 2023 11:30 AM
KAA yasema ‘ajali’ ya ndege iliyoripotiwa ilikuwa ya majaribio ya kujipima

KAA yasema ‘ajali’ ya ndege iliyoripotiwa ilikuwa ya majaribio ya kujipima

NA MWANDISHI WETU

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Nchini (KAA) imesema ‘ajali’ ya ndege iliyoripotiwa leo Jumatano asubuhi imekuwa ya majaribio ya kujipima uwezo wake kushughulikia majanga na matukio ya dharura endapo yanaweza kutokea.

KAA kupitia kwa taarifa imesema shughuli za uokozi wakati wa majaribio hayo zimeendeshwa kwa utaratibu mzuri na hakuna aliyeumia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi.

KAA imesema usalama wa wafanyakazi, ndege na abiria ni wa umuhimu mkubwa.

Mkurugenzi Mkuu wa KAA Bw Alex Gitari amesema majaribio kama hayo huwa na umuhimu mkubwa.

“Tunaupa usalama kipaumbele, hivyo kufanya majaribio ya ajali na kujipima uwezo wetu ni uamuzi wa busara. Ninapongeza wafanyakazi wote waliojitolea kuhakikisha majaribio hayo yanakuwa na ufanisi mkubwa,” amesema Bw Gitari.

  • Tags

You can share this post!

Mukumu: Machogu aahidi fidia ya Sh400,000 kwa kila familia...

Waziri Kindiki: Shakahola ina makaburi mengi

T L