• Nairobi
  • Last Updated June 2nd, 2023 9:28 PM
Raila Odinga akiri kutambua Bottom-Up

Raila Odinga akiri kutambua Bottom-Up

Na SAMMY WAWERU

KINARA wa Azimio Raila Odinga amerai wabunge wa Kenya Kwanza ‘wanaojali maslahi ya Wakenya’ kuungana naye kuangusha mapendekezo ya nyongeza ya ushuru (VAT) na kodi.

Akitoa msimamo wa Azimio Jumatatu, Mei 8, 2023 kuhusu Mswada wa Fedha 2023, Bw Raila aliapa kushawishi wabunge wa upinzani kuurambisha sakafu.

Alitaja mswada huo Kaman mapendekezo mabaya kwa uchumi wa nchi na unaopaswa kukataliwa.

“Tutapinga Mswada huo, kupitia wabunge wa Azimio,” alisema Waziri Mkuu huyo wa zamani.

“Ninaamini kuna wabunge wa Kenya Kwanza wanaopenda Wakenya na wanajali maslahi yao, waungane nami kuangusha mapendekezo yanayotolewa na serikali,” alielezea.

Mswada wa Fedha 2023 unapendekeza nyongeza ya VAT kwa bidhaa kama vile petroli, mishahara (kugharamia ujenzi wa makazi ya bei nafuu) na biashara zinazoendelezwa kidijitali.

Endapo mswada huo utapitishwa na bunge, VAT ya mafuta ya petroli itaongezeka kutoka asilimia 8 hadi 16.

Nyongeza hiyo itaashiria mzigo mzito kwa mlipa ushuru, hususan wananchi wa mapato ya chini ikizingatiwa kuwa gharama ya maisha ni ghali.

Kwa mara ya kwanza, Bw Raila kwenye kikao na wanahabari Nairobi aliskika kutambua mfumo wa serikali ya Rais William Ruto, wa ‘bottom-up’ aliotumia kama mojawapo ya sera kushawishi wapigakura kumchagua Agosti 9, 2023.

“Wabunge wanaoamini mfumo wa bottom-up, waungane nami kutetea Wakenya,” akasema.

Odinga aidha amekuwa akipinga uhalali wa serikali ya sasa, akihoji haikuchaguliwa kihalali.

Katika uchaguzi mkuu 2022, alimenyana na Rais Ruto kupitia muungano wa Azimio.

Aliibuka wa pili, kesi aliyowasilisha katika Mahakama ya Juu zaidi Nchini kupinga kura za urais ikifutilia mbali malalamishi yake.

  • Tags

You can share this post!

Gachagua: Machifu 20 na manaibu kufutwa kwa kushindwa...

Masaibu: Pasta Ezekiel ‘afungiwa’ akaunti zake...

T L