• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:53 PM
Rais Ruto awateua makatibu wawili wa wizara kujaza nafasi zilizotokea

Rais Ruto awateua makatibu wawili wa wizara kujaza nafasi zilizotokea

NA CHARLES WASONGA 

RAIS William Ruto mnamo Mei 31, 2023 amependekeza watu wawili wapya kwa uteuzi kuwa Makatibu wa Wizara.

Bi Salome Wairimu Muhia-Beacco ameteuliwa kuwa Katibu wa Idara ya Magereza katika Wizara ya Usalama wa Ndani, kuchukua pahala pa Esther Ngero aliyejiuzulu juzi.

Bi Muhia-Beacco ni Wakili wa Mahakama Kuu mwenye tajriba ya miaka 26. Pia amewahi kuhudumu katika kampuni ya kutengeneza saruji ya Bamburi Cement na kampuni za bima za AIG, Phoenix East Africa na ile ya ICEA.

Naye Bi Anne Njoki Wang’ombe amependekezwa kwa uteuzi kuwa Katibu wa Wizara atakayesimamia Idara ya Usimamizi wa Utendakazi katika Afisi ya Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi.

Wakati huu Bi Wang’ombe anahudumu kama Meneja wa Mpango wa Malipo ya Uzeeni katika Mamlaka ya Ushuru Nchini (KRASPS).

Kwenye taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari, Jumatano, Mei 31, 2023 Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei amesema Rais Ruto amefanya teuzi hizo kufuatia mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma (PSC).

“Majina ya wawili hao yatawasilishwa katika Bunge la Kitaifa kupigwa msasa na wakiidhinishwa watajiunga na maafisa wengine wakuu serikalini,” Bw Koskei akasema.

  • Tags

You can share this post!

Shakahola: Awamu ya pili ya upasuaji maiti yakamilika...

Mzee wa jamii ya Boni adai hakuna cha kujivunia Madaraka Dei

T L