• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 10:30 AM
Serikali yalenga kukusanya Sh4.2 bilioni kila siku

Serikali yalenga kukusanya Sh4.2 bilioni kila siku

NA DANIEL OGETTA

SERIKALI inatarajia kukusanya Sh4.2 bilioni kila siku kuanzia mwaka ujao, 2023, kufuatia kuanzishwa kwa huduma za serikali kwenye mfumo wa kielektroniki.

Hii itawezesha serikali kukusanya Sh1.4 trilioni ifikapo Desemba 2024.

Katika taarifa iliyothibitishwa na Taifa Leo Dijitali, katika kipindi hicho, huduma za uraia mtandaoni zimeongezeka kutoka huduma 397 hadi 13,645, huku watumiaji waliosajiliwa kufikia 12,083,914.

Mwaka jana, 2023, mapato ya serikali kupitia mtandao huo ilikusanya Sh60 milioni kila siku.

Katibu Mkuu wa Huduma za Uhamiaji na Raia, Julius Bitok alisema mapato hayo yamekua, sasa serikali ikikusanya Sh350 milioni kila siku.

Balozi Bitok alisema serikali inatarajia kukusanya mapato ya Sh1 bilioni kila siku mwishoni mwa Desemba 2023.

Kulingana na Katibu wa Baraza la Mawaziri Mercy Wanjau, ambaye pia ni mwenyekiti wa mfumo wa kielektroniki, wizara nyingi, idara na mashirika alisema agizo la rais liliweza kufuatwa.

Vile vile, ameziomba idara zote za serikali kufanya kazi kwa karibu na usimamizi wa kielektroniki ili kuhakikisha kwamba inafuata maagizo kikamilifu.

“Kuhakikisha utiifu wa maagizo unasalia kuwa ajenda ya kudumu katika mikutano yote muhimu inayofanyika ndani ya jalada lako. Hili litakuwa na manufaa kuhakikisha maendeleo na uwajibikaji kufikia makataa,” alisema Bi Wanjau.

Kwenye waraka wa Desemba 1 kwa makatibu wote wa Baraza la Mawaziri, Bi Wanjau alisema sharti maagizo hayo yafuatwe kikamilifu.

Sherehe za mwaka 2022, Siku ya Jamhuri, Rais Ruto aliagiza huduma 5,000 ziwekwe kwenye tovuti hiyo katika kipindi cha miezi sita (ifikapo Juni 30, 2023).

Kiongozi wa nchi aliagiza kufungwa kwa mifumo ya malipo ambayo haijateuliwa na kuhamishwa kwa nambari ya malipo ya 222222 iliyotangazwa kwenye gazeti la serikali.

 

  • Tags

You can share this post!

Wezi wa nguo wanaojifanya maafisa wa Kenya Power

Vijana waonywa dhidi ya ngono bila kinga

T L