• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 4:47 PM
Seth Panyako ajiuzulu naibu mwenyekiti UDA akidai imefeli Wakenya

Seth Panyako ajiuzulu naibu mwenyekiti UDA akidai imefeli Wakenya

Na WINNIE ONYANDO

NAIBU Mwenyekiti wa Chama cha UDA Seth Panyako, amejiuzulu kutokana na msimamo wa serikali kuhusu ushuru na gharama ya juu ya maisha.

Bw Panyako alitangaza kujiuzulu kwake kutoka kwa chama tawala wakati wa hafla ya mazishi ya aliyekuwa mwanasiasa Joseph Hamisi huko Kakamega Jumamosi, Mei 26, 2023.

Akiwahutubia waombolezaji, Bw Panyako ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Muungano wa Kitaifa wa Wauguzi Nchini (KNUN) alieleza kuwa anajiondoa kutoka chama hicho kutokana na msimamo wake wa kupinga ushuru wa Hazina ya Nyumba na kupanda kwa gharama ya maisha.

Alisisitiza kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kikao kifupi na kiongozi wa chama chake Rais William Ruto.

“Nilizungumza na Rais saa saba mchana na ilionekana nisingeweza kuendelea na jukumu langu kwa kuwa napinga hazina ya nyumba na pia nawaunga Wakenya kuhusu gharama ya juu ya maisha,” alisema Bw Panyako.

 

 

  • Tags

You can share this post!

Nakuru yapokea mitungi ya Oksijeni kuboresha huduma za afya

Messi aweka rekodi mpya ya ufungaji mabao bara Ulaya

T L