• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 7:20 PM
Shakahola: Awamu ya pili ya upasuaji maiti yaanza leo Alhamisi

Shakahola: Awamu ya pili ya upasuaji maiti yaanza leo Alhamisi

NA ALEX KALAMA

AWAMU ya pili ya upasuaji wa maiti za wahanga wa imani potovu inatarajiwa kuanza leo Alhamisi katika mochari ya Hospitali Kuu ya Malindi.

Shughuli hiyo inafunguliwa rasmi na Waziri wa Usalama wa Ndani Prof Kithure Kindiki.

Tayari Prof Kindiki amewasili Malindi, Kaunti ya Kilifi ili kufungua rasmi shughuli hiyo.

Maiti 129 za wahanga wa imani potovu zilizofukuliwa kutoka kwenye makaburi ndani ya msitu wa Shakahola ndizo zitafanyiwa upasuaji kwenye awamu hii ya pili.

Operesheni ingali inaendelea kwenye msitu huo na jana Jumatano mtu mmoja aliokolewa, idadi ya waliookolewa ikipanda na kufika 91.

Kulingana na ripoti iliyotolewa kwa vyombo vya habari, idadi jumla ya waliokamatwa kuhusiana na matukio ya eneo hilo ni watu 34.

Ripoti hiyo aidha imeonyesha kuwa familia 613 zilizopoteza wapendwa wao eneo hilo zimejitokeza na kusajiliwa huku 19 zikiunganishwa na wapendwa wao.

Idadi ya walioangamia inasalia watu 240.

  • Tags

You can share this post!

Azimio yataka msajili wa vyama vya kisiasa atoke

Shakahola: Kindiki afungua rasmi awamu ya pili ya upasuaji...

T L