• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 11:38 AM
Shakahola: Awamu ya pili ya upasuaji maiti yakamilika katika mochari ya Malindi

Shakahola: Awamu ya pili ya upasuaji maiti yakamilika katika mochari ya Malindi

NA ALEX KALAMA

WATAALAMU wa upasuaji wa maiti wametamatisha awamu ya pili ya upasuaji wa maiti za Shakahola mnamo Jumatano katika mochari ya Hospitali Kuu ya Malindi.

Jumla ya miili 16 imefanyiwa uchunguzi.

Akizungumza baada ya kukamilisha shughuli hiyo, mwanapatholojia mkuu wa serikali Dkt Johansen Oduor ameeleza kuwa yule mtu aliyefariki katika hospitali ya Malindi kwa kukataa chakula, alifariki kutokana na kufeli kwa figo zake kutokana na ukosefu wa maji ya kutosha mwilini.

“Leo tumefanyia miili 16 upasuaji ambapo miili 11 ilikuwa ya watu wazima, miili minne ikiwa ya watoto na mwili mmoja hatukuweza kutambua kwa ajili ya kuainisha kwa sababu ulikuwa umeharibika sana. Nao mwili mmoja ulikuwa wa mtu aliyeaga dunia kwa wadi baada kukataa kutibiwa na kula,” amesema Dkt Oduor.

Aidha imebainika kuwa watu 10 walifariki kwa ukosefu wa maji na chakula. Nao uchunguzi wa maiti tano umeshindwa kudhihirisha kilichosababisha vifo vyao vyenyewe kwa sababu miili ilikuwa imeharibika vibaya.

Kufikia sasa maafisa hao wamefanya upasuaji wa miili 131 katika awamu ya pili na idadi jumla ikiwa ni miili 243 ambayo imefanyiwa uchunguzi tangu kuanza kwa shughuli hiyo mwanzoni mwa Mei 2023.

Sasa ufukuaji wa maiti unatarajiwa kurejelewa tena kuanzia Jumanne wiki ijayo.

  • Tags

You can share this post!

Washukiwa wa uvamizi wa shamba la familia ya Kenyatta...

Rais Ruto awateua makatibu wawili wa wizara kujaza nafasi...

T L