• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 9:50 AM
Soko la utalii lapigwa jeki kutokana na wawekezaji wa Kiarabu kutua nchini

Soko la utalii lapigwa jeki kutokana na wawekezaji wa Kiarabu kutua nchini

Na WINNIE ATIENO

BODI ya Utalii nchini (KTB) na wawekezaji katika sekta ya utalii kutoka mataifa ya Kiarabu wameungana kupiga jeki soko la Kenya la utalii.

Wadau hao walisema ndege ya moja kwa moja kutoka Mombasa hadi Dubai itaendelea kukuza utalii katika nchi za Kiarabu.

Mwaka jana serikali ilianzisha ndege ya moja kwa moja kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi Mombasa hadi Dubai kupitia shirika la usafiri la Kenya Airways ili kukuza utalii wa Pwani.

Kulingana na takwimu kutoka KTB, soko la utalii katika mataifa ya Mashariki ya Kati zimeonyesha uwezo mkubwa wa kukuza sekta ya utalii hapa nchini.

“Kutoka Januari hadi Machi 2023 tumeshuhudia asilimia 20 ya ongezeko la watalii (4,070) ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu ambapo tulipokea wageni 3,328. Ndiyo maana sasa KTB imekita kambi nchi za Kiarabu kusaka watalii na kuuza soko letu,” alisema Mkurugenzi wa KTB, Bw Victor Shitakha.

Alisema kuwa wanapania kuongeza idadi ya watalii wa nchi hizo kwa asilimia 30 ifikapo Juni 2024.

“Tutafanya hilo kupitia ushirikiano na shirika la usafiri wa ndege la Kenya Airways, wawekezaji wa usafiri na utalii,” aliongeza.

Akiongea kwenye sherehe ya kuwakaribisha wageni hao, kutoka Uarabuni katika eneo la Fort Jesus, Bw Shitakha alisema soko la Uarabuni lina uwezo wa kukuza utalii humu nchini.

Kampuni ya ndege ya Kenya Airways husafiri mara nne kwa wiki kutoka Mombasa hadi Dubai.

“Ni usafiri wa saa tano kutoka Kenya hadi Dubai. Masaa ya kusafiri kati ya nchi hizi mbili yamepunguzwa baada ya kuanzishwa kwa safari za moja kwa moja na kampuni ya ndege ya Kenya Airways. Vile vile, tunalenga Uarabuni sababu ni watalii ambao wanatumia pesa sana,” alisema Bw Shitakha.

Afisa wa mauzo wa kampuni ya Kenya Airways, Bi Peninah Nyokabi, alisema ushirikiano wao na wawekezaji wa utalii utakuza sekta hiyo.

“Tulialika wadau wa utalii kutoka Dubai waje katika vivutio vyetu vya utalii ili waweze kuonyesha ulimwengu mzima umuhimu wa kuzuru Kenya hasa eneo la Pwani ambalo lina vivutio vingi ikiwemo mbuga za kitaifa za Wanyama wa pori, fuo, na utamaduni wa kale,” alisema Bi Nyokabi.

Wakala wa usafiri kutoka Dubai, Bi Swapna Shabeer alisema Kenya inastahili kukuza soko lake kwa kuandaa maonyesho.

“Inasikitisha kuwa tunajua kuhusu mbuga ya Wanyama pori ya Maasai Mara lakini hatujui chochote kuhusu Pwani, inaonyesha kuna pengo kubwa ambalo liko wazi. Pwani ina vivutio vingi vya utalii ni muhimu wahsika dau wakutumi furha hii kukuza soko hili,” alisema.

Walipata fursa ya kutembelea mbuga za Wanyama pori ikiwemo Maasai Mara, Amboseli, Tsavo Mashariki na Magharibi, ufuo wa Pwani na hoteli kadhaa.

 

  • Tags

You can share this post!

Polisi watwaa vifaa vya kanisa la Ezekiel Odero

Raha tele Vihiga wakinyanyua ubingwa wa Ligi Kuu

T L