• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 AM
Ugavi wa mali ya Bilionea Tob Cohen wasimamishwa na mahakama

Ugavi wa mali ya Bilionea Tob Cohen wasimamishwa na mahakama

Na RICHARD MUNGUTI

FAMILIA ya marehemu Tob Cohen imepata pigo kubwa mahakama iliposimamisha ugavi wa mali yake huku wosia mbili zikichupuza katika kesi ya urithi kati ya mjane wake na nduguze.

Jaji Muruge Thande alisitisha ugawaji wa mali ya Cohen, raia wa Uholanzi hadi kesi iliyoshtakiwa na Sarah Wairimu Cohen isikizwe na kuamuliwa. Jaji Thande aliamuru ugavi wa mali ya Cohen usiendelee hadi itakapojulikana ni wosia upi kati ya ule uliokuwa na wakili mwenye tajriba ya juu Chege Kirundi ama ni ule wa Sarah Wairimu.

Baada ya Cohen kufariki Bw Kirundi aliwaita watu wa familia ya Cohen na kuufungua Wosia aliokuwa amemtayarisha akiwa na mfanyabiashara huyo wa kimataifa. Katika wosia huo , mali zake marehemu alikuwa amewapa ndugu na dada zake na nduguze na Sarah hakupewa kitu.

Kupitia kwa wakili Philip Murgor,Sarah anadai wosia alionao Bw Kirundi ni feki. Nayo familia ya Cohen inadai Sarah anayeshtakiwa kwa mauaji ya mumewe ameghushi Wosia aliowasilisha mahakamani. Jaji Thande aliamuru Wosia hizo mbili ziwasilishwe mahakamani kukaguliwa.

Kesi hiyo ya urithi itasikizwa Juni 2022.

You can share this post!

Apania kutinga hadhi ya kimataifa katika uigizaji miaka...

Mulomi atangaza azma yake kurithi kiti cha Ojaamong

T L